Thursday, November 20, 2014

Halmashauri ya Ikungi yakusanya zaidi ya shilingi billion 2 ndani ya miezi 3 kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Celestine Yunde, akizungumza kwenye kikao cha kawaida cha baraza la madiwani.Kulia ni makwamu mwenyekiti, Ali Mwanga na wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ikungi,Hassan Tanti na anayefuatia ni Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri wilaya Ikungi, Mahammud Nkya.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi, Mahammud Nkya, akitoa taarifa yake mbele ya kikao cha kawaida cha baraza la madiwani kilichofanyika Ikungi. Kulia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Ikungi, Celestine Yunde na kushoto ni mwenyekiti CCM wilaya ya Ikungi, HassanTanti.

Diwani wa kata ya Mungaa jimbo la Singida mashariki (CHADEMA),Alex  Matheo, akitoa mchango wake kwenye kikaa cha kawaida cha madiwani kilichofanyika Ikungi.
Diwani viti maalum kata ya Ikungi (CHADEMA), Teddy Gadhau, akichangia mada kwenye kikao cha baraza la madiwani.Teddy alidai kwamba fedha za mfuko wa jimbo la Singida mashariki, zinatumika vizuri na kwa malengo yaliyokusudiwa,tofauti na mawazo ya baadhi ya watu wanavyofikiri.
Diwani wa kata ya Iseke wilaya ya Ikungi mkoa Singida (CHADEMA) Emmanuel Jingu, akiomba kura kwa ajili ya kujaza pengo la nafasi ya Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Ikungi  lililoachwa wazi na Alli Nkhangaa aliyejiunga na  CHADEMA akitokea CCM.Jingu aliambulia kura tatu kati ya 31 zilizopigwa.

HALMASHAURI ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida, imekusanya mapato ya zaidi ya shilingi 2.9 bilioni kutoka vyanzo vyake mbalimbali vya mapato, kati ya Julai na Septemba 30 mwaka huu.

Makusanyo hayo ni sawa na asilimia 15 ya lengo la kukusanya zaidi ya shilingi 19.1 bilioni kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015


Hayo yamesemwa na mweka hazina wa halmashauri hiyo mpya, Celestine Mutashobya, wakati akitoa taarifa yake mbele ya kikao cha kawaida cha madiwani kilichofanyikia kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo.

Alisema halmashauri hiyo imekusanya zaidi ya shilingi 76.9 milioni kutoka kwenye mapato yake ya ndani.Kiasi hicho ni sawa na asilimia 12 ya lengo la kukusanya zaidi ya shilingi 628.4 milioni.

Mutashobya alisema kuwa hadi sasa serikali kuu bado haijaipatia halmashauri hiyo fidia ya kodi na ushuru uliofutwa. Hata hivyo halmashauri bado inatarajia kupewa ruzuku ya shilingi 590 milioni ikiwa ni fidia ya kodi na ushuri uliofutwa.

“Serikali kuu imetupatia ruzuku ya kulipia mishahara zaidi ya shilingi bilioni mbili kati ya lengo la zaidi ya shilingi bilioni 11. Pia serikali kuu imetupatia ruzuku ya kugharamia matumizi yasiyo ya mishahara zaidi ya shilingi 1.4 bilioni na kwenye miradi tumepatiwa zaidi ya shilingi 563.5 milioni kati ya lengo la zaidi ya shilingi 5.4 bilioni”,alifafanua mweka hazina huyo.


Kwa mujibu wa mweka hazina huyo,halmashauri hiyo imelipa kata zaidi ya shilingi 7 milioni ikiwa ni marejesho ya aslimia 20 ya marejesho ya mapato na shilingi zingine milioni tisa wamelipia pango la ofisi ya makao makuu ya halmashauri kwa kipindi cha miezi sita

No comments:

Post a Comment