Mkuu wa Kitengo cha usalama barabarani Wilaya ya Singida (DTO), Antony Sempanga akimwonesha Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani Mkoa wa Singida Akhlan Ghalib,kifaa cha kisasa cha kupima mwendo kasi (speed radar) wakati wa akitoa taarifa juu ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani Mkoa wa Singida kwa waandishi wa habari (hawapo pichani).
Mkuu wa Kitengo cha usalama barabarani Wilaya ya Singida (DTO), Antony Sempanga akiwaonesha waandishi wa habari jinsi speed radar ya kisasa inavyofanya kazi.
Mkuu wa Kitengo cha usalama barabarani Wilaya ya Singida (DTO), Antony Sempanga akiwaonesha waandishi wa habari jinsi speed radar ya kisasa inavyofanya kazi.
Antony akiwa na kifaa cha kupima mwendo kasi.
Antony akionesha waandishi wa habari nama ya kupokea sms kwa njia ya mtandao kutoka kwenye speed radar kwenda kwenye simu ya mkononi.
Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani, Akhlan Ghalib akizungumza na vyombo vya habari juu ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani jana.
Mwandishi wa habari, Damiano Mkumbo akitambulisha wana habari kwa kamati ya usalama barabarani, Mzee Mkumbo pia ni mjumbe kwenye kamati hiyo anayewakilisha vyombo vya habari.
WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kuwa mstari wa mbele katika kukemea tabia ya madereva wa mabasi kuendesha kwa mwendo kasi ili kupunguza ajali za barabarani.
Changamoto hiyo imetolewa mjini hapa na Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani Mkoa wa Singida Akhlan Ghalib wakati alipokuwa akizungumza juu ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani kwenye ofisi za klabu ya waandishi wa habari Mkoani hapa, (Singida Press Club).
Ghalib alisema waandishi wa habari ni nguzo muhimu katika kutumia kalamu zao ipasavyo ili kukemea vitendo hivyo ambavyo vinahartarisha usalama wa wananchi, pamoja na kusababisha vifo vinavyoweza kuepukika.
“Nyie mna nafasi kubwa sana katika kutusaidia kwenye jambo hili pamoja na kwamba serikali inaliona hili na kulitilia mkazo kwa hawa madereva kuendesha kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani, pia kalamu yenu ni muhimu sana, tusaidieni. “ Alisema Ghalib.
Kwa upande wake Kaimu Katibu wa usalama barabarani ambaye pia ni mkuu wa kitengo cha usalama barabarani Wilaya ya Singida (DTO), Antony Sempanga alisema hivi sasa jeshi la polisi limejipanga ipasavyo katika kudhibiti mwendo kasi wa mabasi mbalimbali.
Sempanga alisema polisi Mkoani Singida imepatiwa jumla ya vifaa 18 kwa ajikli ya kusoma mwendo kasi(Speed Radar) vya kisasa ambavyo vinaweza kurekodi na kupiga picha madereva wakiwa wanaendesha kwa mwendo kasi.
“Vifaa hivi ni vya kisasa kabisa na vina memory card yenye GB 32 sasa tumeandaa utaratibu mpya kabisa kwamba wale wanaotumia vifaa hivyi hawatakuwa wanavaa sare za polisi bali watakuwa wamevalia kiraia na kutakuwa na askari mbele ambao watapata taarifa juu ya dereva aliyezidisha mwendo, ka hatua zaidi za kisheria.”Aklisema na kuongeza …….
“Kwa hiyo hata kama dreva atabisha juu ya kosa lake wale, waliorekodi tutawaita kwa ushahidi, na vizuri zaidi pia kutakuwa na namna ya kurusha picha kwa njia ya mtandao kwenye simu ya askari kutoka kwa wale waliovalia kiraia wanaotumia vifaa hivi.” Alisisitiza Sempanga.
Hata hivyo alisema kuna changamoto nyingi zinajitokeza zaidi kwa waendesha bodaboda kwa kutokuwa na mwitikio mkubwa wa kuvaa helment wao pamoja na abiria wao, hasa saa za jioni, na pia wananchi kuibuka na kujichulia sheria mkononi pindi ajali inapotokea.
No comments:
Post a Comment