Thursday, September 17, 2015

Serikali kuboresha zaidi mazingira ya kufanyia shughuli za wajasiriamali mkoani Singida.

Meneja mradi wa kuwajengea uwezo wafanyabiashara wadogo,Florentina Sallah, akitoa nasaha zake kwenye ufunguzi wa mafunzo ya siku tano yanayohudhuriwa na wafanyabiashara wadogo 150 wa mkoa wa Singida.Wa kwanza kulia ni Mkuu wa mkoa wa Singida,D k.Parseko Kone na anayefuatia ni,Dk.Willhelm Ngasamiaku,mhadhiri wa uchumi idara ya uchumi chuo kikuu cha Dar-es-salaam.
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone,akizungumza kwenye uzinduzi wa mafunzo ya siku tano yanayohudhuiwa na wafanyabiashara wadogo 150 yanayoendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha maendeleo ya wananchi mjini hapa. Dk.Kone ameahidi kuwa serikali mkoani hapa itaendelea kuwajengea mazingira mazuri wafanyabiashara hao, ili shughuli zao ziwe za tija zaidi.
Mhadhiri wa uchumi idara ya uchumi chuo kikuu cha Dar-es-salaam, Dk.Wilhelm Ngasamiaku,akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa mafunzo ya wafanyabiashara wadogo 150 wa mkoa wa Singida yanayoendelea kwenye chuo cha maendeleo ya wananchi mjini hapa.Wa pili kulia ni mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone na wa kwanza kulia ni mkuu wa wilaya ya Singida,Iddi Amanzi. Kushoto ni Meneja mradi wa kuwajengea uwezo wafanyabiashara wadogo,Florentina Sallah.

Baadhi ya wafanyabiashara wadogo mkoani Singida, wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone (hayupo pichani),wakati akizindua mafunzo ya wafanyabiashara hao.
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone,(wa pili kulia walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na wakufunzi wa mafunzo ya wafanyabiashara wadogo.Kulia aliyeketi ni mkuu wa wilaya ya Singida,Idd Amanzi.Wa tatu kushoto waliosimama,ni Meneja mradi wa kuwajengea uwezo wafanyabiashara wadogo,Florentina Sallah na aliyeketi kushoto, ni mhadhiri wa uchumi chuo kikuu cha Dar-es-salaam,Dk.Wilhelm Ngasamiaku.

SERIKALI mkoani Singida, imeahidi kuendelea kuboresha mazingira ya kufanyia shughuli za wajasiriamali mbalimbali, ili shughuli zao ziweze kuwa zenye tija zaidi.

Ahadi hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone,wakatai akizindua mafunzo ya wafanyabiashara wadogo 150 mkoani hapa yanayoendelea kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) mjini hapa.

Alisema serikali kwa upande wake imewajengea wajasiriamali mazingira rafiki na mazuri ya kufanyia shughuli zao zikiwemo za kilimo cha mbogamboga na za kuzalishaji wa bidhaa mbalimbali.

“Miaka michache iliyopita, serikali imeweza kugoresha na kujenga barabara za kiwango cha lami zenye urefu wa zaidi ya kilometa mia nne. Pia imehakikisha mawasiliano mazuri ya simu za viganjani yanapatikana kwa urahisi karibu sehemu zote za mkoa wetu wa Singida”, alifafanua Dk.Kone.

Akiongezea, alisema wajasiriamali mkoni hapa,kwa sasa wanatumia barabara za lami kufikisha mazao na bidhaa zao kwenye masoko ya uhakika kwa urahisi na kwa muda mfupi mno.

“Wajasiriamali vile vile wanatumia simu zao za viganjani kutafutia masoko nadani na nje ya nchi.Kwa kutumia mawasiliano hayo wamekuwa wakiagiza bidhaa na kuletewa mahali walipo bila wao kusumbuka kwa kuzifuatia”,alisema.

Aidha, Dk.Kone alisema serikali mkoani hapa itajitahidi kuhakikisha wajasiriamali wanapata mazingira salama na utulivu kwa ajili ya shughuli zao na kuwasaidia kurasimisha biashara zao,ili klungeza tija na kipato chao pia.

Katika hatua nyingine,mkuu huyo wa mkoa, amewataka wajasiriamali hao wawe mabalozi wazuri kwa wenzao ambao hawajapata bahati ya kupata mafunzo hayo.

“Ni imani yangu kuwa mtakwenda kuwafundisha wenzenu faida na umuhimu wa kurasimisha biashara zao huku mkiwaeleza hasara za kufanya biashara katika mazingira yasiyo rasmi”,alisema mkuu huyo wa mkoa.

Dk.Kone ametumia fursa hiyo kuushukuru uongozi wa ESAURP (Eastern and Southern African Universities Research Programe) kwa kugharamia mafunzo hayo na kuuomba uendelee kuleta mafunzo zaidi ya aina mbalimbali.

Awali meneja wa mradi wa kuwajengea uwezo wafanyabiashara wadogo pamoja na kuwarasimisha, Florentina Sallah, alisema mradi huo unatekelezwa katika mikoa 10 hapa nchini.


Alisema madhumuni na malengo ya mradi huo,ni pamoja na kuwapatia mafunzo wafanyabiashara wadogo yatakatowasaidia kuondokana na kufanya biashara katika mfumo usio rasmi, na kuanza kutumi mfumorasmi utakaowasaidfia kuwatambulisha na wadau mbalimbali wakiwemo wa taasisi za kifedha.

No comments:

Post a Comment