Saturday, August 24, 2013

Mapato katika halmashauri ya Singida yaporomoka kwa sababu mbalimbali ikiwemo bodaboda kugomea ushuru.

 Makamu Meya wa manispaa ya Singida na Diwani wa kata ya Mungumaji Bw. Hassan Mkata (kushoto) akiongoza kikao cha Baraza la Madiwani.Kulia ni kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Singida.
 Diwani wa kata ya Misuna manispaa ya Singida, Hamisi Kisuke akichangia mada wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa manispaa ya Singida kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi mjini Singida.
Baadhi ya Madiwani wa Manispaa ya Singida wakifuatilia kwa makini kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi mjini.

Makusanyo ya mapato ya baadhi ya vyanzo vya mapato vya halmashauri ya manispaa ya Singida, yameporomoka kutokana na sababu mbalimbali na kusababisha manispaa hiyo kushindwa kufikia malengo yake.

Imedaiwa katika vyanzo hivyo vilivyoporomoka kwa makusanyo ya mapato, manispaa ilijiwekea lengo la kukusanya mapato ya zaidi ya shilingi milioni 797.5 kwa mwaka wa fedha wa 2012/2013, lakini hadi Februari mwaka huu, ilikuwa imekusanya zaidi ya shilingi milioni 217.6 tu.

Hayo yamesemwa na Kaimu Meya wa manispaa ya Singida Hassan Mkata, mbele ya kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha maendeleo ya wananchi mjini Singida.

 Ametaja baadhi ya vyanzo hivyo kuwa ni pamoja na ushuru wa pikipiki (bodaboda) ambao lengo lilikuwa ni kukusanya shilingi milioni 24, lakini zilizokusanywa ni shilingi 235,000 sawa na asilimia moja ya lengo.

Amesema  “Wamiliki wa bodaboda wamegoma kulipa ushuru huo. Magogoro huu umewasilishwa mbele ya ofisi ya mkuu wa wilaya ya Singida na ofisi ya mkurugenzi inafuatilia ili kupata muafaka juu ya suala hili”.

Mkata ametaja chanzo kingine ni cha kodi ya thamani ya majengo ambacho kilikuwa kiipatie manispaa zaidi ya shilingi milioni 118.8, lakini zilizokusanywa ni zaidei ya shilingi milioni 22.3 sawa na aslimia 19 tu,

Amesema sababu iliyosababisha kuporomoka kwa kodi ya thamani ya majengo ni mwamko  mdogo wa wananchi kulipa kodi za majengo kwa hiari.

Mkata amesema “Tulijipangia kukusanya zaidi ya shilingi

Thursday, August 22, 2013

Wazawa wa mkoa wa Singida wenye uwezo washauriwa kuwekeza mkoani humo ili kuuletea maendeleo.

                                                   Bango la Katala Beach Hotel.
Sehemu ya majengo ya Katala Beach Hotel iliyopo kandokando ya Ziwa Singidani.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu Juma Ali Simai (wa sita kutoka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurungezi Mkuu wa Katala Beach Hotel bw. Kitila Katala (mstari wa mbele mwenye koti rangi ya kijivu) pamoja na viongozi mbalimbali na wananchi wa manispaa ya Singida. 

Mkurugenzi Mkuu wa Hoteli ya Katala Beach ya mjini Singida Kitila Katala, amewataka wazawa wa mkoa wa Singida walioko nje ya mkoa wenye uwezo kiuchumi, kuangalia uwezekano wa kuwekeza vitenga uchumi mbalimbali ili kuharakisha upatikanaji wa maendeleo katika mkoa wao.

Katala ametoa changamoto hiyo wakati akizungumza juu ya umuhimu wa wazawa wa mkoa wa Singida walioko nje ya mkoa, kushirikiana na ndugu zao kuuendeleza mkoa wa Singida ili usiendelee kubaki nyuma kimaendeleo.

Amesema uzoefu unaonyesha wazi kwamba wazawa wengi wa mkoa wa Singida wenye uwezo kiuchumi, wamekuwa wakiwekeza nje ya mkoa wao, kitendo kinachochangia mambo mengi ikiwemo mkoa kuendelea kuwa wa kwanza nchini kwa sifa ya umaskini.

Amesema ili mkoa uweze kupiga hatua kimaendeleo ikiwemo kuondoa sifa mbaya ya kuwa mkoa wa kwanza kwa umaskini ni lazima wazawa wa mkoa wa ndani na nje ya mkoa, kushikamana na kushirikiana katika kuuletea mkoa maendeleo endelevu yanayokwenda na wakati.

Kuhusu hotel yake ya Katala Beach, Mkurugenzi huyo amesema anatarajia ujenzi wa hotel yake hadi utakapokamilika, utamgharimu zaidi ya shilingi bilioni 2.5.

Hotel hiyo ya Katala Beach iliyopo kando kando ya ziwa Singidani, imezinduliwa rasmi na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Juma Ali Simai Agosti 21 mwaka huu.


Simai alimpongeza Katala kwa uamuzi wake wa kuwekeza mkoani kwake na kudai kuwa kitendo hicho ni cha kizalendo mno, na kuwataka wazawa wengine wa mkoa wa Singida kuiga uzalendo ulioonyeshwa na Katala wa kuendelea mkoa wake.

Wito watolewa kwa waandishi wa habari kushirikiana na Wataalam wa Afya kufanya tafiti ili kuboresha sekta ya Afya nchini.

 Mwezeshaji wa mafunzo ya masuala ya Afya waJjumuiya ya vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC),Dk.Ahmed Twaha (wa pili kulia) akitoa wito kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha) kushirikiana na Wataalam wa Afya kufanya tafiti katika masuala ya Afya zitakazosaidia kuboresha Sekta ya Afya. Dk.Twaha ametoa wito huo kwenye kikao kifupi kati ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dk.Dorothy Gwajima na waandishi wa habari.
 Mganga mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Dorothy Gwajima akitoa ufafanuzi wa masuala ya Afya kwa Waandishi wa Habari (hawapo kwenye picha) waliomtembelea ofisini kwake.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria kikao kati yao na mganga mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Dorothy Gwajima kilichofanyikia ofisini kwa mganga mkuu huyo.

Wanachama wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Singida, wameshauriwa kushirikiana na wataalam wa Afya kufanya tafiti mbalimbali zitakazosaidia kudhibiti/kutokomeza magonjwa ambayo ni kero kwa wananchi.
Changamoto hiyo imetolewa na mwezeshaji wa masuala ya Afya Dk.Ahmed Twaha wakati akizungumza kwenye kikao kifupi kati ya Mganga Mkuu wa mkoa wa Singida na waandishi wa habari.

Amesema vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika mapambano dhidi ya adui maradhi kama vikitumika ipasavyo.

“Mkitumia vizuri kalamu zenu katika kuielimisha jamii kupitia Redio, Tv au Makala katika magazeti juu ya athari mbalimbali zinazosababishwa na maradhi itasaidia jamii kuchukua hatua za kujihadhari na magonjwa na kwa ujumla na mtakuwa mmeusaidia Mkoa kuwa na wakazi wenye Afya bora”,amesema.

Pia amewataka kujenga utamaduni wa

Monday, June 24, 2013

Mwanafunzi wa kike mkoani Singida adaiwa kutelekeza mtoto wa miezi mitano.

Mkuu wa wilaya ya Singida, mwalimu Queen Mlozi akiwa amempakatia mtoto wa kiume ambaye inadaiwa kutelekezwa kwenye pagara la nyumba na mama yake ambaye anasoma chuo cha uhasibu tawi la Singida.Mtoto huyo mwenye umri wa miezi mitano, amehifadhiwa wodi sita (b) katika hospitali ya mkoa mjini Singida.
Mwanafunzi wa kike wa chuo cha uhasibu tawi la mkoa wa Singida ambaye

Sunday, June 2, 2013

Watoto wawili wa familia moja wauawa kikatili mkoani Singida baada ya kulawitiwa na watu wasiojulikana.

 Afisa mtendaji wa kata ya Iguguno Josia Pangani akizungumzia tukio la kulawitiwa na kisha kunyongwa hadi kufa wanafunzi wawili wa familia moja wa shule ya msingi Lukomo wilaya ya Mkalama.
 Mama mzazi wa watoto waliobakwa na kisha kunyongwa hadi kufa Veronica Nuru mkazi wa kijiji cha Lukomo wilaya ya Mkalama, akizungumzia tukio la kuuawa kikatili watoto wake.
Makaburi walikozikwa wanafunzi wawili waliolawitiwa na kisha kunyongwa hadi kufa.

Watoto wawili wa familia moja wameuawa kikatili  mkoani Singida baada ya kulawitiwa na  watu wasiojulikana,  kisha  kunyongwa kabla ya milii yao  kwenda kufungwa kwenye mti porini.

Watoto hao wametajwa kuwa ni Esta Daudi  (14)  na  Anita Shila (9)  wote wanafunzi wa darasa la saba na  tatu katika shule ya msingi Lukomo kata ya Iguguno wilaya ya Mkalama mkoani Singida.

Afisa mtendaji wa kata hiyo Josia  Pangani, amesema tukio hilo limetokea majira ya saa  12 jioni wakati watoto hao  wa kike wakiwa wanachunga mifugo kwenye pori jirani na nyumbani kwao.

Pangani amesema  baada ya  muda  wa kurejesha  mifugo  zizini kufika, wazazi wa watoto hao  walishangaa kutowaona watoto wala mifugo, hali iliyosababisha kuanza juhudi za kuwatafuta.

Amesema juhudi hizo hazikuweza kuzaa matunda siku hiyo hadi kesho yake walipoikuta miili ya watoto hao ikiwa imefungwa kwenye mti.

Baada ya uchunguzi  wa kitaalamu kufanyika, ilibainika kuwa walibakwa, kunyongwa shingo, kisha kufungwa vitambaa usoni na watu wasiojulikana.

Habari za kipolisi zinasema  kuwa watu wawili akiwemo baba mzazi wa watoto waliouawa

Saturday, May 25, 2013

Kliniki tembezi yazinduliwa wilaya ya Iramba mkoani Singida kwa lengo la kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto.

 Mganga mkuu wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida. Dk.Japhet Simeo akitoa taarifa yake katika hafla ya uzinduzi wa kliniki tembezi katika wilaya hiyo yenye lengo la kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto.Uzinduzi huo umefanyika katika zahanati ya kata ya Ndago wilaya ya Iramba.
 Mkuu wa wilaya ya Iramba Yahaya Nawanda, akizungumza kwenye uzinduzi uliofana  wa kliniki tembezi inayotarajiwa kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto.Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Singida,mwalimu Queen Mlozi na kulia ni mkuu wa wilaya ya Manyoni, Fatuma Toufiq.
 Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida,Yahaya Nawanda (kulia) akizindua kliniki tembezi kwa wilaya hiyo, kwa kupima mama mjamzito Mary Kiula.
 Mkulima wa kijiji cha Sinziligi kata ya Ndago wilaya ya Iramba,Michael Mguna akisaidiwa kubeba mtoto wake Leonard na mama mmoja ambaye sio mke wake.Michael alidai kuwa mke wake alibanwa na shughuli za nyumbani na hivyo yeye akalazimika kumpekeka mtoto wao kliniki kwa mujibu wa ratiba.Mkuu wa wilaya ya Iramba,Yahaya Nawanda amewataka wanaume wote kujenga utamaduni wa kuwasindikiza wake zao kwenda kliniki.

Baadhi ya akina mama wajawazito na wasio wajawazito wa kata ya Ndago wilaya ya Iramba,waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa kliniki tembezi wilayani humo.Kliniki hiyo, imedaiwa kuwa ni ya kwanza hapa nchini.