Sunday, November 3, 2013

Mkuu wa wilaya ya Singida Mwl. Mlozi afunga mafunzo ya Mgambo.

Mkuu wa wilaya ya Singida, mwalimu Queen Mwashinga Mlozi akikagua Gwaride ikiwa ni sehemu ya kufunga mafunzo ya askari Mgambo wa manispaa ya Singida. Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Peoples klabu mjini Singida.
Baadhi ya askari Mgambo 90 wakitembea kwa mwendo wa taratibu kama sehemu ya kufunga mafunzo yao.
Askari mgambo waliohitimu,wakitoa heshima zao kwa mgeni rasmi wa ufungaji mafunzo hayo,mkuu wa wilaya ya Singida,mwalimu Queen Mwashinga Mlozi (hayupo kwenye picha).
Askari mgambo wakitoa heshima kwa mgeni rasmi wa kufunga mafunzo yao mkuu wa wilaya ya Singida ,mwalimu Queen Mwashinga Mlozi.

Thursday, October 31, 2013

Shule ya msingi Ikungi yazindua ufundishaji kwa njia ya TEHAMA.

Mkuu wa wilaya ya kungi mkoani Singida, Manju Msambya akizindua mitambo ya kufundishia kwa njia ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) katika shule ya msingi Ikungi mchanganyiko.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi (mwenye skafu) akipewa maelezo na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ikungi mchanganyiko, Olivary Kamili,juu ya mitambo ya kufundishia TEHAMA.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, Manju Msambya akiangalia screen inayoonyesha namna somo linavyotolewa kupitia TEHAMA.

Shule ya Msingi Ikungi mchanganyiko wilaya ya Ikungi mkoani Singida imezindua rasmi ufundishaji wa kisasa kupitia mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kuwawezesha wanafunzi kutumia vifaa mbalimbali katika mawasiliano na kujiendeleza kielimu.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo,Mwalimu Mkuu wa shule hiyo,Olivary Kamili amesema mfumo huo wa ufundishaji pia utawawezesha wanafunzi kwenda na wakati katika kujifunza.

Akifafanua amesema mfumo huo utawajengea mazingira mazuri wanafunzi kuwa na tabia ya udadisi ambayo itapelekea wawe wagunduzi.

“Kupitia somo la TEHAMA wanafunzi watajenga tabia ya kujifunza kupitia udadisi wa mambo mbali mbali hivyo itasaidia kupata vijana ambao watakuwa na uwezo wa kufanya tafiti za uhakika”,amesema Mwalimu Kamili.

 Aidha, amesema kutokana na umuhimu wa somo la TEHAMA ameishauri Serikali ilipe kipaumbele kwa kuhakikisha shule zote zinanufaika na somo hilo.

 “Somo la TEHAMA linarahisisha sana upatikanaji wa elimu bora na yenye mafanikio makubwa.Napendekeza serikali iangalie namna ya kuboresha somo hili ili liweze kuwa na

Wednesday, October 30, 2013

Kero za wananchi zinahitaji majadiliano ya pamoja.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi, Protace Magayane akizungumza kwenye mahafali ya 13 ya shule ya sekondari Sepuka.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi, Protace Magayane (mwenye miwani) akimkabidhi cheti cha kuhitimu kidato cha nne mmoja kati ya 58 wa shule ya sekondari Sepuka.

Baadhi ya wazazi/walezi wa wanafunzi wanaotarajiwa kumaliza kidato cha nne mwaka huu wa shule ya sekondari ya Sepuka wilaya ya Ikungi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida Protace Magayane amewahimiza wazazi  na walezi kujenga utamaduni wa kujadili kwa pamoja kero zinazowakabili katika maeneo yao na kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu.

Magayane ametoa changamoto hiyo hivi karibuni wakati akizungumza kwenye kilele cha mahafali ya 13 ya shule ya sekondari ya Sepuka, Jimbo la Singida Magharibi.

Akifafanua amesema katika mikutano ya kitongoji, Kijiji na Kata wananchi hawana budi kuweka bayana kero na shida zao na kuzipa vipaumbele.

Akitoa mfano, Magayane amesema katika majadiliano hayo ya pamoja, wanaweza kubainisha kero zinazowakabili katika sekta mbalimbali zikiwemo za sekta ya barabara, maji, elimu na afya.

“Wananchi kwa ushirikiano na viongozi wenu,baada ya kujadiliana,muweke mikakati ya pamoja ya namna ya kutumia nguvu zenu wenyewe katika kutatua kero hizo”,alifafanua Mkurugenzi huyo.

Aidha amewataka katika majadiliano hayo waweke utaratibu wa matumizi bora ya raslimali za ardhi, maliasili, madini na zinginezo ili

Diwani wa Chadema kizimbani kwa kuvunja ofisi ya kijiji na kuiba.

Diwani wa CHADEMA kata ya Iseke jimbo la Singida magharibi Emmanuel Jackson Jingu (45) akiwa kwenye chumba cha mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida, akisubiri kusomewa kesi yake ya kuvunja na kuiba kwenye ofisi ya serikali ya kijiji cha Nkhoiree.Diwani Emmanuel alishinda nafasi hiyo hivi karibuni kwenye chaguzi ndogo zilizofanyika hivi karibuni.

Diwani wa Kata ya Iseke Tarafa ya Ihanja (CHADEMA) Jimbo la Singida Magharibi, Emmanuel Jackson Jingu (45) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Singida akikabiliwa na mashitaka mawili ya kuvunja ofisi ya kijiji cha Nkhoiree.

Mapema Mwendesha Mashitaka Mwanasheria wa Serikali, Petrida Muta alidai mbele ya Hakimu Asha Mwetindwa kuwa mnamo septemba 20 mwaka huu saa 8.30 mchana mshitakiwa alivunja nyumba kwa lengo la kuiba mali huku akijua wazi kwamba kitendo hicho ni kinyume cha sheria.

Mwendesha Mashitaka Muta alimsomea mshitakiwa shitaka la pili kuwa siku hio hiyo na wakati huo huo mshitakiwa baada ya kuvunja mlango wa nyumba inayotumiwa na serikali ya kijiji cha Nkhoiree aliweza kuiba vifaa mbalimbali vyenye thamani vya thamani ya shilingi 298,000.

Alitaja vifaa hivyo na thamani yake kwenye mabano kuwa ni vocha (hazikuweza kuelezwa ni za nini)(32,000),vitabu vya risiti (12,000),cash book (10,000),risiti za ushuru (28,000),hati za malipo (4,000),vitabu vya ushuru (10,000),risiti za zahanati (28,000) na madumu tupu 100 (150,000).

Mshitakiwa alikana mashitaka hayo na ameenda rumande baada ya kukosa mdhamini wa ahadi ya shilingi

Tuesday, October 29, 2013

UNYAMA:WANAWAKE 3 WADAIWA KUMUUA MWENZAO KWA KUDAI HAKI YA MWANAE.

Mtuhumiwa wa mauaji Tabu Jumanne (50) mkazi wa Kibaoni Singida mjini (katikati anayekwepa kamera) akiwa kwenye chumba cha mahakama ya wilaya ya Singida akisubiri kusomewa shitaka la kuumuawa Fatuma Shaban. Tabu anakabiliwa na shitaka la kumuuawa Fatuma, akishirikiana na binti zake Halima Swedi (anayejificha mwenye fulana nyekundu) na Mwamvua Yusuph baada ya mwanamke huyo kumdai Tabu amlipe mshahara binti yake aliyekuwa akifanya kazi za ndani.

Askari polisi wakiwa na mahabusu wakiwapeleka mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Singida kusomewa mashitaka yanayowakabili.

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 50 na watoto wake wawili wa kike wakazi wa Kibaoni mjini Singida wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Singida wakituhumiwa kumuuawa Fatuma Shaban maarufu kwa jina la mama Rabeca.

Washitakiwa hao ni Tabu Jumanne na binti zake Halima Swedi na Mwamvua Yusuph.

Mapema Mwendesha Mashitaka Sajenti wa Polisi Godwel Lawrance alidai mbele ya  Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Singida, Flora Ndale kuwa mnamo julai nne mwaka huu majira ya jioni huko katika kitongoji cha Mahembe kata ya Kinadi Manispaa ya Singida washitakiwa kwa pamoja walimpiga Fatuma Shaban sehemu mbalimbali za mwili wake.

Lawrance amesema kipigo hicho kilisababisha kifo cha Fatuma pale pale.

Washitakiwa hawakutakiwa kujibi cho chote kwa vile Mahakama hiyo ya Wilaya haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji Kesi hiyo inatarajiwa kutajwa tena Novemba sita mwaka huu.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa siku ya tukio Fatuma alienda nyumbani kwa mshitakiwa Tabu kudai fedha za

Wanaokataa kuchangia Maendeleo ya sekta ya Elimu ni Walemavu wa akili.

Mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Ikungi mchanganyiko wilaya ya Ikungi,Naftali Gukwi akitoa nasaha zake kwenye ufunguzi wa sherehe ya mahafali ya 62 ya shule hiyo yaliyofanyika  mkoani Singida.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ikungi mchanganyiko,Olivary Kamili akitoa taarifa yake kwenye kilele cha mahafali ya 62 ya wahitimu 179 wa darasa la saba.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida,Manju Msambya akizungumza kwenye mahafali ya 62 ya shule ya msingi Ikungi mchanganyiko. Wa kwanza kulia ni mwenyekiti wa kijiji cha Ikungi,Machemba Mghewa na kushoto ni mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Naftali Gwae.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida,Manju Msambya, akimkabidhi cheti cha kuhitimu elimu ya msingi mmoja wa wanafunzi 179 waliohitimu.
Baadhi ya wahitimu wa wa darasa la saba wa shule ya msingi Ikungi wilaya ya Ikungi wakiwa na vyeti vyao vya kuhitimu elimu ya msingi baada ya kukabidhiwa na mkuu wa wilaya ya Ikungi,Manju Msambya.\

Wakazi wa wilaya ya Ikungi mkoani singida ambao wamekubali kudanganyika na kuamua kugoma kuchangia maendeleo yao yakiwemo ya sekta ya elimu hao ni walemavu wa akili imeelezwa.

 Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Manju Msambya, wakati akizungumza kwenye mahafali ya 62 ya shule ya msingi Ikungi mchanganyiko Jumla ya wanafunzi 179 wamehitimu elimu ya msingi.

 Amesema wilaya hiyo ya Ikungi na hasa jimbo la Singida mashariki imepandikizwa sera mbaya ya kuwataka wananchi kutokuchangia kabisa maendeleo yao.

 “hapo awali uzoefu unaonyesha wazi wananchi wakiwemo wa jimbo la Singida mashariki, walikuwa wanachangia kwa hali na mali maendeleo yao bila shuruti. Mfano mzuri ni kwamba wamejenga kwa moyo mmoja shule za sekondari za kata na zingine, kuwa na vyumba vya madarasa vya ziada.”,amesema Msambya.

 Akifafanua zaidi, DC huyo amesema baada ya sera hiyo isiyo na mashiko wala tija kupandikizwa wananchi hawataki tena kuchangia wala

Friday, October 25, 2013

MKOA WA SINGIDA WADHIBITI VITENDO VYA UHALIFU.

                                     MRAKIBU WA POLISI BW.JAMES KASUSURA

                         PICHA ZOTE TOKA MAKITABA YA SINGIDAYETUBLOG.

Mkoa wa Singida ni miongoni mwa mikoa minne nchini iliyofanikiwa kupambana na vitendo vya uhalifu kwa kiwango kikubwa kwa kipindi cha hivi karibuni.

Mrakibu  wa Polisi kutoka makao makuu Dar es salaam kitengo cha maadili James Kasusura amesema hayo wakati akizungumza na washiriki wa kikao cha siku maalum ya polisi kilichofanyika katika ukumbi wa Aquar manispaa ya Singida.

Kasusura ameyataja makosa yaliyopungua kuwa ni makosa dhidi ya ubinadamu ambayo yamepungua kwa asilimia 35, makosa dhidi ya mali yamepungua kwa asilimia 18, makosa dhidi ya maadili yamepungua kwa sailimia 13, na makosa dhidi ya usalama barabarani yamepungua kwa asilimia 12.

Amesema kupungua kwa makosa hayo kumetokana na ushirikiano baina ya raia na vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Singida, hivyo kutoa wito wa kuendelezwa kwa ushirikiano huo na hatimae kukomesha vitendo hivyo kabisa.