Friday, October 25, 2013

MKOA WA SINGIDA WADHIBITI VITENDO VYA UHALIFU.

                                     MRAKIBU WA POLISI BW.JAMES KASUSURA

                         PICHA ZOTE TOKA MAKITABA YA SINGIDAYETUBLOG.

Mkoa wa Singida ni miongoni mwa mikoa minne nchini iliyofanikiwa kupambana na vitendo vya uhalifu kwa kiwango kikubwa kwa kipindi cha hivi karibuni.

Mrakibu  wa Polisi kutoka makao makuu Dar es salaam kitengo cha maadili James Kasusura amesema hayo wakati akizungumza na washiriki wa kikao cha siku maalum ya polisi kilichofanyika katika ukumbi wa Aquar manispaa ya Singida.

Kasusura ameyataja makosa yaliyopungua kuwa ni makosa dhidi ya ubinadamu ambayo yamepungua kwa asilimia 35, makosa dhidi ya mali yamepungua kwa asilimia 18, makosa dhidi ya maadili yamepungua kwa sailimia 13, na makosa dhidi ya usalama barabarani yamepungua kwa asilimia 12.

Amesema kupungua kwa makosa hayo kumetokana na ushirikiano baina ya raia na vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Singida, hivyo kutoa wito wa kuendelezwa kwa ushirikiano huo na hatimae kukomesha vitendo hivyo kabisa.

No comments:

Post a Comment