Mwenyekiti wa kamati ya shule ya msingi Ikungi mchanganyiko wilaya ya Ikungi,Naftali Gukwi akitoa nasaha zake kwenye ufunguzi wa sherehe ya mahafali ya 62 ya shule hiyo yaliyofanyika mkoani Singida.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ikungi mchanganyiko,Olivary Kamili akitoa taarifa yake kwenye kilele cha mahafali ya 62 ya wahitimu 179 wa darasa la saba.Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida,Manju Msambya akizungumza kwenye mahafali ya 62 ya shule ya msingi Ikungi mchanganyiko. Wa kwanza kulia ni mwenyekiti wa kijiji cha Ikungi,Machemba Mghewa na kushoto ni mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Naftali Gwae.
Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida,Manju Msambya, akimkabidhi cheti cha kuhitimu elimu ya msingi mmoja wa wanafunzi 179 waliohitimu.
Baadhi ya wahitimu wa wa darasa la saba wa shule ya msingi Ikungi wilaya ya Ikungi wakiwa na vyeti vyao vya kuhitimu elimu ya msingi baada ya kukabidhiwa na mkuu wa wilaya ya Ikungi,Manju Msambya.\
Wakazi wa wilaya ya Ikungi mkoani singida ambao wamekubali kudanganyika na kuamua kugoma kuchangia maendeleo yao yakiwemo ya sekta ya elimu hao ni walemavu wa akili imeelezwa.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Manju Msambya, wakati akizungumza kwenye mahafali ya 62 ya shule ya msingi Ikungi mchanganyiko Jumla ya wanafunzi 179 wamehitimu elimu ya msingi.
Amesema wilaya hiyo ya Ikungi na hasa jimbo la Singida mashariki imepandikizwa sera mbaya ya kuwataka wananchi kutokuchangia kabisa maendeleo yao.
“hapo awali uzoefu unaonyesha wazi wananchi wakiwemo wa jimbo la Singida mashariki, walikuwa wanachangia kwa hali na mali maendeleo yao bila shuruti. Mfano mzuri ni kwamba wamejenga kwa moyo mmoja shule za sekondari za kata na zingine, kuwa na vyumba vya madarasa vya ziada.”,amesema Msambya.
Akifafanua zaidi, DC huyo amesema baada ya sera hiyo isiyo na mashiko wala tija kupandikizwa wananchi hawataki tena kuchangia wala
kujenga vyumba vitatu vya maabara kwa kila shule ya sekondari.
“Jimbo la Singida mashariki karibu shule zote za sekondari, ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara nI asilimia sifuri. Wamekubali kudanganywa kwamba serikali ina fedha za kutosha kufanya kazi hiyo. Waliokubaliana na hilo, hao pamoja na kuwa walemavu wa akili pia ni wachovu wa kufikiri”,amesema.
Hata hivyo,Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka wananchi wachukue haraka maamuzi ya kubadilika vinginevyo wilaya ya Ikungi itakuwa ya kwanza kuzalisha wanafunzi mbumbumbu kwa kukosa elimu ya sayansi.
Aidha Msambya alidai kwamba kuna kila dalili zinazoashiria kwamba wanafunzi wa wilaya hiyo kuwa wafanyakazi wa ndani kwenye nyumba za wasomi kutokana na wazazi wao kuwaandalia mazingira ya kufeli mitihani.
Awali Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Olivary Kamili amesema kuwa shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri katika ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba, kwa miaka mitatu mfululizo.
Alifafanua, Kamili amesema mwaka 2010 ufaulu wa wanafunzi wa darasa la saba, ulikuwa asilimia 79.3 mwaka 2011 asilimia 76.8 na mwaka jana asilimia 93.5.
Katika kuonyesha kwamba wakazi wa jimbo la Singida Mashariki wamegoma kuchangia maendeleo yao, katika harambee iliyofanywa juzi na DC Msambya ya kuchangia ujenzi wa bweni la wanafunzi walemavu, zaidi ya wazazi/walezi 400 waliohudhuria mahafali hayo, walichanga shilingi 62,000 taslimu tu, na fedha nyingi zilikuwa ni za sarafu (coins).
Kwa upande wake Msambya, aliahidi kuchangia mifuko 20 ya saruji na trip 20 za mchanga.
No comments:
Post a Comment