Tuesday, October 29, 2013

UNYAMA:WANAWAKE 3 WADAIWA KUMUUA MWENZAO KWA KUDAI HAKI YA MWANAE.

Mtuhumiwa wa mauaji Tabu Jumanne (50) mkazi wa Kibaoni Singida mjini (katikati anayekwepa kamera) akiwa kwenye chumba cha mahakama ya wilaya ya Singida akisubiri kusomewa shitaka la kuumuawa Fatuma Shaban. Tabu anakabiliwa na shitaka la kumuuawa Fatuma, akishirikiana na binti zake Halima Swedi (anayejificha mwenye fulana nyekundu) na Mwamvua Yusuph baada ya mwanamke huyo kumdai Tabu amlipe mshahara binti yake aliyekuwa akifanya kazi za ndani.

Askari polisi wakiwa na mahabusu wakiwapeleka mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Singida kusomewa mashitaka yanayowakabili.

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 50 na watoto wake wawili wa kike wakazi wa Kibaoni mjini Singida wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Singida wakituhumiwa kumuuawa Fatuma Shaban maarufu kwa jina la mama Rabeca.

Washitakiwa hao ni Tabu Jumanne na binti zake Halima Swedi na Mwamvua Yusuph.

Mapema Mwendesha Mashitaka Sajenti wa Polisi Godwel Lawrance alidai mbele ya  Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Singida, Flora Ndale kuwa mnamo julai nne mwaka huu majira ya jioni huko katika kitongoji cha Mahembe kata ya Kinadi Manispaa ya Singida washitakiwa kwa pamoja walimpiga Fatuma Shaban sehemu mbalimbali za mwili wake.

Lawrance amesema kipigo hicho kilisababisha kifo cha Fatuma pale pale.

Washitakiwa hawakutakiwa kujibi cho chote kwa vile Mahakama hiyo ya Wilaya haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji Kesi hiyo inatarajiwa kutajwa tena Novemba sita mwaka huu.

Kwa mujibu wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa siku ya tukio Fatuma alienda nyumbani kwa mshitakiwa Tabu kudai fedha za
mshahara wa binti yake aliyekuwa ameajiriwa kufanya kazi za ndani.

Inadaiwa kitendo cha Fatuma (marehemu) kumdai mshitakiwa Tabu malipo ya mshahara wa binti yake kilizua ugomvi na ndipo Tabu kwa ushirikiano wa binti zake waliamua kumpiga mama huyo na kusababisha kifo chake papo hapo.

No comments:

Post a Comment