Saturday, March 15, 2014

Mwanafunzi wa kidato cha kwanza afa maji.

Mwili wa mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Ipembe mjini Singida Rashid Said (16) (kushoto) na wa kijana ambaye hajafahamika jina aliyekuwa anajaribu kumwokoa mwanafunzi.Vijana hao wawili waliofariki dunia Machi 08 mwaka huu saa nane mchana ,mwanafunzi huyo amefariki dunia baada ya Mtumbwi waliokuwa wameupanda kupigwa na upepo na wao kutumbukia ndani ya maji.
Mwili wa mwanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya sekondari Ipembe Rashid Said, ukiingizwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa mjini Singida.

MWANAFUNZI wa kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Ipembe mjini hapa,Rashid Saidi (16) amefariki dunia baada ya mtumbwi aliokuwa umeupanda ziwani, yeye na baadhi ya wanafunzi wenzake kupigwa na upepo mkali na kusababisha mtumbwi kupinduka na wao kutumbukia kwenye maji.

Kijana mmoja ambaye sio mwanafunzi na jina lake bado halijapatikana,alijitolea kumwokoa mwanafunzi huyo,lakini naye kwa bahati mbaya alifariki dunia baada ya kunywa maji mengi na kuzama ziwani.

Inadaiwa kuwa wanafunzi hao baada ya kumaliza kipindi cha’tuition’ shuleni kwao,kama kawaida yao walienda ‘pikiniki’ katika ziwa la Kindai na kuanza kuogelea pembeni mwa ziwa hilo.

Askari kutoka kikosi cha zima moto mjini hapa,Bahati Hemed,amesema kwa mujibu wa taarifa alizopewa na mashuhuda wa tukio hilo,ni kwamba baada ya wanafunzi hao kumwagwa ndani ya maji,baadhi ya wanafunzi
walifanikiwa kujiokoa na Rashid ambaye hana uzoefu wa kuogelea,alizama ndani ya maji.

Amesema wanafunzi hao baada ya kutoka nje ya ziwa,walimwomba kijana mmoja ambaye alikuwa na umri mkubwa aingie ziwani ili akamwokoe mwanzao.

“Yule kijana aliyejitolea kumwokoa mwanafunzi,alipokaribia alikotumbukia mwanafunzi huyo,na yeye mambo yalimwendea vibaya na hivyo kutumbukia ndani ya maji na kusababaisha na yeye apoteze maisha yake”alisema Bahati kwa masikitiko.


Alisema baada ya hapo waliweza kuita wavuvi ambao walifika na nyavu na kuwaza kutoa miili hiyo miwili kutoka ndani ya ziwa Kindai.

No comments:

Post a Comment