Wednesday, October 8, 2014

Walipwa fidia ya mil 263/- kupisha ujenzi wa chuo.

Mkurugenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania tawi la Singida, Hassanal Issaya akiwa ofisini kwake akitekeleza majukumu yake ya kila siku.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha utumishi wa  umma Tanzania tawi la Singida wakiwa kwenye darasa wakati wa masomo.

Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha utumishi wa umma Tanzania tawi la Singida, wakiwa kwenye darasa la mafunzo ya hati mkato (shorthand).
Baadhi ya vyumba vya madarsa vya chuo cha umma Tanzania tawi la Singida.

CHUO cha utumishi wa umma  Tanzania tawi la mkoa wa Singida,limetumia shilingi 263 milioni kulipa fidia kwa wakazi wa kijiji cha Sasu kata ya Mungumaji manispaa ya Singida,ili waweze kupisha ujenzi wa chuo hicho mwaka wa fedha ujao.

Hayo yamesemwa  na Mkurugenzi wa chuo hicho, Hassanal Issaya, wakati akizungumza na MOblog ofisini kwake, juu ya maendeleo ya chuo hicho likichoanzishwa julai 2011.

Alisema zoezi la ulipaji wa fidia,limefanyika kwa amani na utulivu kwa  kuwa kila mwananchi alilipwa kulingana na stahiki zake, kwa mujibu wa sheria ya fidia.


Issaya alisema kwa sasa chuo kinaendelea na utaratibu wa kupata hati ya eneo hilo litakalojengwa chuo lenye ukubwa wa ekari 78.6.

“Tumepanga katika mwaka wa fedha ujao pamoja na mambo mengine,tutafute mzabuni atakaye chora michoro ya matumizi ya  eneo kulingana na mahitaji ya chuo.Lengo ni kuhakikisha kuwa chuo kinakuwa na majengo yake ya kisasa kabisa”,alisema Issaya kwa kujiamini.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo,chuo hicho kwa sasa kimepanga kwenye majengo ya mtu binafsi ambapo kwa mwaka,wanalipa shilingi 80 kwa pango.

Kuhusu changamoto zingine,Issaya alitaja kuwa ni pamoja na uhaba wa watumishi wa kudumu.

Akifafannua, alisema Chuo kwa sasa kina jumla ya watumishi 65,kati yao 35 sawa na aslimia 54,ni wa kudumu.Watumishi 30 ambao ni sawa na aslimia 46,ni walimu ambao huajiriwa kwa mikataba ya muda wa miezi sita.Walimu hawa wa muda,huwa wanahama mara kwa mara wanapopata kazi sehemu zingine na kuacha pengo.


Alisema kitendo cha walimu hao kuhama mara kwa mara,kunaathiri sana shughuli mblimbali za chuo na kupelekea kuanza kutafuta wengine wa kuzipa pengo.

No comments:

Post a Comment