Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na tukio la maafa ya mvua kubwa iliyosababisha vifo.
MVUA kubwa zilizoanza kunyesha mkoani Singida zimeanza kuleta maafa baada ya watu watano kuhofiwa kufa maji kutokana na gari waliolokuwa wakisafiria kusombwa na maji ya mto.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, SACP Geofrey Kamwela amesema tukio hilo limetokea Desemba saba mwaka huu saa 3:30 asubuhi huko katika mto wa Nzalala kijiji cha Kisimba tarafa ya Kisiriri wilayani Iramba.
Amesema siku ya tukio, abiria 16 waliokuwa wakitoka kijiji cha Doromoni kwa kutumia Landrover 110 TDI lenye namba za usajili T.499 ATR, lilisombwa na maji ya mto wakati dereva wake akijaribu kuvuka mto Nzalala.
Akifafanua, amesema walimpofika kwenye mto huo abiria hao walimwomba dereva huyo asubiri maji ya mto yapungue ili waweze kuvuka lakini dereva huyo alikataa kwa madai maji ni machache.
“Wakati gari hilo lilipofika katikati ya mto, lilizimika ghafla na wakati huo huo maji ya mto yaliongezeka na kulifunika gari. Dereva na kondakta waliweza kufanikiwa kutoka na kukimbilia kusikojulikana”
Aidha, amesema abiria 11 waliweza kuokolewa na wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Iramba na watano hadi sasa haijulikani iwapo wamekufa ndani ya landrover au wamesomba na maji na kupelekwa kusikojulikana.
Katika hatua nyingine, Kamanda Kamwela, ametoa wito kwa madereva wa vyomba vya moto, baiskeli na watembea kwa miguu kuchukua tahadhari wakati wa kuvuka mito au mabonde kipindi hiki cha mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.
Alitumia fursa hiyo kushauri mamlaka zinazohusika kutengeneza madaraja kwenye mito au mabonde badala ya kuweka zege ambalo husaidia tu katika kipindi cha kiangazi.
“Aidha nashauri abiria nao wasikubali
kujazwa kwenye vyombo vya usafiri tofauti na uwezo hali wa gari” amesema.
No comments:
Post a Comment