Tuesday, December 4, 2012

Diwani kata ya Ikungi Singida (CHADEMA) amesema ripoti ya uwajibikaji haitochakachuliwa kamwe.

 Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida Manju Msambya (aliyesimama) akitangaza kuahirishwa kwa mkutano wa mrejesho wa ripoti ya uwajibikaji katika halmashauri ya wilaya ya Singida.Wa tatu kutoka kushoto ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Singida na wa pili kushoto ni makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Singida Alli Nkhangaa.
 Pichani juu na chini ni Baadhi wa wadau wa maendeleo wa halmashauri ya wilaya ya Singida wakimsikiliza kwa makini mkuu wa wilaya ya Ikungi,Manju Msambya (hayupo pichani) wakati akiahirisha mkutano wa mrejesho wa ripoti ya uwajibikaji.

 Mmoja wa maafisa kutoka shirika lisilo la kiserikali la Sikika akikusanya ripoti zilizosababisha kuahirishwa kwa mkutano wa mrejesho wa ripoti ya uwajibikaji katika halmashauri ya wilaya ya Singida.
Kiongozi wa timu ya shirika lisilo la kiserikali la Sikika Mahindi Simon akieleza kusikitishwa kwake kuahirishwa kwa mkutano wa mrejesho wa ripoti ya uwajibikaji.


Diwani wa viti maalum (CHADEMA) tarafa ya Ikungi wilayani Ikungi mkoani Singida Tedi Daghau, amesema pamoja na halmashauri ya wilaya ya Singida kusogeza mbele mkutano wa mrejesho wa ripoti ya uwajibikaki, haitakuwa na ubavu wa  ‘kuichakachua’ ripoti hiyo kwa lengo la.....

Jamii yaombwa kusaidia makundi maalumu yasiyojiweza.

 Mkuu wilaya Iramba-Singida, Yahaya Nawanda akikabidhi msaada wa madaftari kwa mwanafunzi Hilda Samwel (12) uliotole na vikundi vitatu vya jumuiya ya kuweka na kukopeshana (SELC).
DC Iramba Yahaya Nawanda akimkabidhi mwanafunzi Jacob David (11) wa shule msingi Kiomboi hospitali msaada wa madaftari uliotole na vikundi vitatu vya jumuiya ya kuweka na kukopeshana (SELC).


Mkuu wa wilaya Iramba mkoani Singida, Yahaya Nawanda ameitaka jamii kusaidia makundi yasiyojiweza, wakiwemo watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi, ili kujenga moyo wa upendo baina yao.
Nawanda alisema hayo wakati akikabidhi vifaa mbalimbali vya shule msingi, kwa ajili ya wanafunzi wa shule sita  za watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi, wilayani humo.
Msaada huo ulitolewa na.....

Monday, December 3, 2012

.Kamati ya Siasa ya CCM mkoa wa Singida yachagua wajumbe wake na kutoa ujumbe kwa wataalam wa kilimo kuhakikisha pembejeo zinawafikiwa wakulima kwa wakati.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindai akitoa taarifa yake ya uchaguzi wa kamati ya siasa ya mkoa kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha)


Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Singida kimechagua kamati yake ya siasa mkoa katika uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindai, amewataja wajumbe wa kamati hiyo, kuwa ni

Wilaya ya Iramba Mkoani Singida yangoza kwa maambukizi ya VVU kwa kipindi cha Januari hadi Septemba 2012.

 Mratibu wa TACAIDS mkoa wa Singida Edson Mdala akitoa taarifa yake kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika kimkoa Singida mjini.
 Kaimu mkuu wa mkoa wa Singida na DC wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi akihutubia wananchi waliohudhuria maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika kwenye kituo cha zamani cha mabasi mjini Singida.
 Kaimu mkuu wa mkoa wa Singida,Queen Mlozi (wa kwanza kulia) akiwa amewasha mshumaa kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika kimkoa Singida mjini.Wa pili kulia ni meya wa manispaa ya Singida Sheikh Salum Mahami.
 Mratibu wa shirika la PSI mkoa wa Singida Daniel Mainoya (mwenye maiki) akitoa maelezo juu ya shughuli zinazofanywa na PSI kwa kaimu mkuu wa mkoa wa Singida Queen Mlozi (wa kwanza kulia).
 Kaimu mkuu wa mkoa wa Singida Queen Mlozi (kulia mwenye suti) akikagua banda la Takukuru wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani zilizofanyika kimkoa Singida mjini.
 Kaimu mkuu wa mkoa wa Singida Queen Mlozi (mwenye suti) akishiriki kutoa burudani na watu wanaoishi na virusi (VVU) wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika kimkoa katika manispaa ya Singida.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika kimkoa manispaa ya Singida.


Wilaya ya Iramba mkoa wa Singida inaongoza kwa maambukizi mapya ya virusi vinavyosababisha ugonjwa hatari wa UKIMWI kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Septemba mwaka huu.
Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone, wakati akizungumza kwenye

Sunday, December 2, 2012

SHARO MILLIONEA ASABABISHA BONGE LA BIFU KATI YA DJ CHOKA NA LADY NAAA AKA MTOTO MLITO.





 Haya ni maneno ambayo lady naaa aka mtoto mlito alimwandikia Dj Choka kwenye BBM

Hichi ndicho DJ CHOKA aliandika kwenye account ya ke ya facebook kumjibu lady naah "UJUMBE HUU UKUFIKIE WEE UNAYEJIITA LADY NAH...Nilikaa kimya na nikakuvumiliaaaaa baada ya kupata ujumbe wako mfupi ulioutuma BBM, ukaona haitoshi jana ukaenda...

Saturday, December 1, 2012

MAITI YA SHARO MILLIONEA ALIKATWA VIDOLE NA VIBAKA...

Watu wa nne wamekamatwa na jeshi la police wakiwa na Baadhi ya vitu alivyokuwa navyo marehemu Sharo Milionea kama vile

TAZAMA JINSI SHARO MILLIONEA ALIVYOPATA AJALI.

 Gari alilokua akiendesha Sharo Millionea lilianza kutoka nje ya barabara hapa
 Sehemu gari lilipokwenda kusimama ni pale kwenye watu wengi panaonekana kwa mbali.



 Gari lilivuka hii sehemu na kubinukia kule mbele baada ya hilo daraja dogo ambako ndio liligonga huu mti hapa chini.
 Huu ni mti ambao aliugonga katikati akaukata kuwa vipisi viwili, mwingine ukatupwa mbele ya huu kama unavyoonekana alafu gari ikaenda kubinuka kichwa chini miguu juu kwenye lile eneo la wazi unaloliona kwa mbali baada ya hayo matawi ya huo mti hapo mbele.
                                            kipisi cha pili cha mti aliouvunja katikati.

 Hapa ndipo gari lilikuja kusimama na Sharo Milionea akiwa peke yake kwenye gari alirushwa nje.
Hapa ndipo mwili wa Marehemu ulikutwa baada ya kutupwa kutoka kwenye gari, mashuhuda waliofika kwenye eneo la tukio muda mfupi baada ya ajali wanasema walianza kuwatafuta majeruhi wakidhani ni wengi na hawakumuona mtu yeyote kwenye gari