Mkuu wa wilaya ya Ikungi mkoa
wa Singida Manju Msambya (aliyesimama) akitangaza kuahirishwa kwa
mkutano wa mrejesho wa ripoti ya uwajibikaji katika halmashauri ya
wilaya ya Singida.Wa tatu kutoka kushoto ni mwenyekiti wa halmashauri ya
wilaya ya Singida na wa pili kushoto ni makamu mwenyekiti wa
halmashauri ya wilaya ya Singida Alli Nkhangaa.
Pichani juu na chini ni Baadhi wa wadau wa maendeleo wa halmashauri ya wilaya ya Singida wakimsikiliza kwa makini mkuu wa wilaya ya Ikungi,Manju Msambya (hayupo pichani) wakati akiahirisha mkutano wa mrejesho wa ripoti ya uwajibikaji.
Mmoja wa maafisa kutoka shirika lisilo la kiserikali la Sikika akikusanya ripoti zilizosababisha kuahirishwa kwa mkutano wa mrejesho wa ripoti ya uwajibikaji katika halmashauri ya wilaya ya Singida.
Kiongozi wa timu ya shirika lisilo la kiserikali la Sikika Mahindi Simon akieleza kusikitishwa kwake kuahirishwa kwa mkutano wa mrejesho wa ripoti ya uwajibikaji.

Diwani
wa viti maalum (CHADEMA) tarafa ya Ikungi wilayani Ikungi mkoani
Singida Tedi Daghau, amesema pamoja na halmashauri ya wilaya ya Singida
kusogeza mbele mkutano wa mrejesho wa ripoti ya uwajibikaki, haitakuwa
na ubavu wa ‘kuichakachua’ ripoti hiyo kwa lengo la.....
kulindana na
kuficha uozo.
Akifafanua,
amesema ripoti hiyo ambayo imeandaliwa na shirika lisilo la kiserikali
la Sikika, imeanika wazi uozo pamoja na matumizi mbaya ya raslimali ya
umma, imefahamika vizuri kwa wajumbe waliofika kuhudhuria mkutano huo,
na hawatadanganywa.
Kwa
upande wake kiongozi wa timu ya Sikika Mahindi Simon, amesema kwa
ujumla wameshangazwa na kusikitishwa na uamuzi wa kusogeza mbele mkutano
huo.
Amesema
kwenye ripoti yao, hawakulenga kushutumu kiongozi/mfanyakazi ye yote wa
halmashauri, bali ripoti hiyo inahitaji tu kufafanuliwa kwenye maeneo
yenye utata.
No comments:
Post a Comment