Mkuu wilaya Iramba-Singida, Yahaya Nawanda akikabidhi msaada wa madaftari kwa mwanafunzi Hilda Samwel (12) uliotole na vikundi vitatu vya jumuiya ya kuweka na kukopeshana (SELC).
DC Iramba Yahaya Nawanda akimkabidhi mwanafunzi Jacob David (11) wa shule msingi Kiomboi hospitali msaada wa madaftari uliotole na vikundi vitatu vya jumuiya ya kuweka na kukopeshana (SELC).
DC Iramba Yahaya Nawanda akimkabidhi mwanafunzi Jacob David (11) wa shule msingi Kiomboi hospitali msaada wa madaftari uliotole na vikundi vitatu vya jumuiya ya kuweka na kukopeshana (SELC).
Mkuu
wa wilaya Iramba mkoani Singida, Yahaya Nawanda ameitaka jamii kusaidia
makundi yasiyojiweza, wakiwemo watoto wanaoishi katika mazingira
hatarishi, ili kujenga moyo wa upendo baina yao.
Nawanda
alisema hayo wakati akikabidhi vifaa mbalimbali vya shule msingi, kwa
ajili ya wanafunzi wa shule sita za watoto wanaoishi kwenye mazingira
hatarishi, wilayani humo.
Msaada
huo ulitolewa na.....
vikundi vitatu vya jumuiya ya kuweka na
kukopeshana(SELC), ambavyo kila mwanachama huchangia Shilingi mia tatu,
kwa ajili ya kusaidia makundi mbalimbali yasiyojiweza, wilayani Iramba.
Alibainisha
kuwa, msaada siyo lazima iwe kitu chenye thamani kubwa, bali waweza
kuwa hata wenye thamani ndogo, lakini utakuwa umewaondoa wahitaji kutoka
hatua moja hadi nyingine, kulingana mahitaji yao.
Msaada
huo uliojumuisha sare za shule, madaftari, rula na kalamu, ulitolewa
kwa wanafunzi 74 wa shule sita za msingi katika kata ya Kiomboi, ikiwemo
Kiomboi hospitali, Salala, Lulumba shule ya msingi na Sekondari, Igumo,
Kiomboi Bomani na Kizega.
Vikundi
hivyo vitatu vinavyounda jumuiya hiyo ambavyo kila kimoja kina
wanachama 30 ni Msweki, Loelya na Umoja, ambavyo kwa pamoja
vimeshirikiana kutoa msaada huo wenye thamani ya Sh. 395,000.
Mapema
akisoma risala ya vikundi hivyo kwa mgeni rasmi, katibu wa Msweki,
Johari Manguli alisema wamelazimika kutoa msaada huo kutokana na
wanafunzi hao kufiwa na wazazi wao wote wawilina wengine mzazi mmoja.
Aidha
Johari aliomba wadau, wafadhili na mashirika yenye uwezo kujikita zaidi
kusaidia makundi mbalimbali yenye matatizo, wakiwemo watoto waliofiwa
na wazazi wao na wale wanaoishi kwenye mazingira hatarishi.
Hata
hivyo baadhi ya wazazi na walezi katika hafla hiyo waliofiwa na waume
wao,pia wanafunzi waliopoteza wazazi wao, walieleza kwa masikitiko tabu
na shida wanazopata katika kukabaliana na maisha ya kila siku.
No comments:
Post a Comment