Mratibu wa TACAIDS mkoa wa
Singida Edson Mdala akitoa taarifa yake kwenye kilele cha maadhimisho ya
siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika kimkoa Singida mjini.
Kaimu mkuu wa mkoa wa Singida na DC wa wilaya ya Singida,Queen Mlozi akihutubia wananchi waliohudhuria maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika kwenye kituo cha zamani cha mabasi mjini Singida.
Kaimu mkuu wa mkoa wa Singida,Queen Mlozi (wa kwanza kulia) akiwa amewasha mshumaa kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika kimkoa Singida mjini.Wa pili kulia ni meya wa manispaa ya Singida Sheikh Salum Mahami.
Mratibu wa shirika la PSI mkoa wa Singida Daniel Mainoya (mwenye maiki) akitoa maelezo juu ya shughuli zinazofanywa na PSI kwa kaimu mkuu wa mkoa wa Singida Queen Mlozi (wa kwanza kulia).
Kaimu mkuu wa mkoa wa Singida Queen Mlozi (kulia mwenye suti) akikagua banda la Takukuru wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani zilizofanyika kimkoa Singida mjini.
Kaimu mkuu wa mkoa wa Singida Queen Mlozi (mwenye suti) akishiriki kutoa burudani na watu wanaoishi na virusi (VVU) wakati wa maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika kimkoa katika manispaa ya Singida.
Baadhi ya wananchi waliohudhuria maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika kimkoa manispaa ya Singida.

Wilaya
ya Iramba mkoa wa Singida inaongoza kwa maambukizi mapya ya virusi
vinavyosababisha ugonjwa hatari wa UKIMWI kwa kipindi cha kuanzia
Januari hadi Septemba mwaka huu.
Hayo
yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone, wakati
akizungumza kwenye
kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani
yaliyofanyika kimkoa katika manispaa ya Singida.
Amesema
katika kipindi hicho, wilaya ya Iramba iliongoza kwa kuwa na kiwango
cha maambukizi ya asilimia 4.45 na kufuatiwa na manispaa ya Singida,
iliyokuwa na maambukizi asilimia 4.
Katika
hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na mkuu wa wilaya ya Singida Queen
Mlozi, amesema kuwa halmashauri ya wilaya ya Manyoni, ilikuwa na aslimia
3.8 na halmashauri ya wilaya ya Singida asilimia 3.
Akifafanua
zaidi Dkt. Kone amesema jumla ya watu 4,651 wa wilaya ya Iramba,
walipima afya zao katika kipindi hicho, 207 sawa na asilimia 4.45
waligundulika kuwa na maambukizi vya virusi vinavyosababisha UKIMWI.
No comments:
Post a Comment