Saturday, December 1, 2012

TAZAMA JINSI SHARO MILLIONEA ALIVYOPATA AJALI.

 Gari alilokua akiendesha Sharo Millionea lilianza kutoka nje ya barabara hapa
 Sehemu gari lilipokwenda kusimama ni pale kwenye watu wengi panaonekana kwa mbali.



 Gari lilivuka hii sehemu na kubinukia kule mbele baada ya hilo daraja dogo ambako ndio liligonga huu mti hapa chini.
 Huu ni mti ambao aliugonga katikati akaukata kuwa vipisi viwili, mwingine ukatupwa mbele ya huu kama unavyoonekana alafu gari ikaenda kubinuka kichwa chini miguu juu kwenye lile eneo la wazi unaloliona kwa mbali baada ya hayo matawi ya huo mti hapo mbele.
                                            kipisi cha pili cha mti aliouvunja katikati.

 Hapa ndipo gari lilikuja kusimama na Sharo Milionea akiwa peke yake kwenye gari alirushwa nje.
Hapa ndipo mwili wa Marehemu ulikutwa baada ya kutupwa kutoka kwenye gari, mashuhuda waliofika kwenye eneo la tukio muda mfupi baada ya ajali wanasema walianza kuwatafuta majeruhi wakidhani ni wengi na hawakumuona mtu yeyote kwenye gari
ila baadae mama mmoja ndio akamuona Sharo Milionea akiwa hapa muda mfupi kabla ya kukata roho.

Moja kati ya mashuhuda alisema kwamba kwenye hilo eneo huwa hakutokei ajali za mara kwa mara, kwa miaka zaidi ya 20 aliyoishi hapa ni ajali chache sana zimetokea, hakuna ajali mwaka huu zaidi ya Sharo Milionea ila mwaka jana ilitokea ajali moja ambapo mtoto wa shule aligongwa na basi la Raha Leo na kufariki.

Hili eneo liko umbali wa kama dakika 40 mpaka Tanga mjini na ni dakika 15 tu mpaka kufika nyumbani kwa kina Sharo milionea ambako ndiko Marehemu alikua anaelekea, rafiki yake wa karibu mwigizaji Kitale (anaeigiza kama teja) kasema mara ya mwisho Sharo aliongea nae na akamwambia anakimbia Tanga mara moja kumpelekea mama yake mtaji wa shilingi milioni sita za biashara ambazo alikua nazo wakati huo kwenye gari lakini imefahamika kwamba hizo pesa zimeibwa zote kwenye eneo la ajali.

No comments:

Post a Comment