Friday, September 6, 2013

Walimu waaswa kuzingatia viapo katika usimamiaji wa mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi.

Mkuu wa shule ya msingi Ikungi mchanganyiko, Olivary Kamili akiagalia wanafunzi wakijipanga tayari kuingia madarasani kuanza masomo.

Mkurugenzi Mtendaji wa kwanza wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida,Magayane Protace,amewataka walimu watakaosimamia mtihani wa taifa wa darasa la saba mwaka huu,kujiepusha na vitendo ambavyo ni kinyume na viapo vyao.

Magayane ametoa tahadhari hiyo mwishoni mwa wiki,wakati akifungua semina iliyohudhuriwa na walimu wa shule za msingi tarafa ya Sepuka,wanaotarajiwa kusimamia mtihani wa taifa wa kumaliza elimu ya msingi mwaka huu.

Alisema kazi ya kusimamia mtihani wa taifa wa darasa la saba,ni lazima kila mwalimu ale kiapo mbele ya

Thursday, September 5, 2013

SEMA na WFP yakabidhi matenki ya kuvunia Maji ya Mvua kwa shule za msingi Sita mkoani Singida

 Meneja mkuu wa shirika la SEMA Ivo Manyaku, akitoa taarifa yake ya ujenzi wa matenki ya kuvunia Maji ya Mvua katika Shule Sita za Msingi za wilaya ya Singida na Ikungi. Matenki hayo yaliyogharimu zaidi ya shilingi 101.9,yanatarajiwa kupunguza kero ya Wanafunzi kupoteza muda mwingi wa masomo katika kutafuta maji.
 Mkuu wa ofisi ndogo ya mpango wa chakula Duniani (WFP) Dodoma, Nima Sitta akihimiza utunzaji wa Matenki ya kuvunia Maji ya Mvua yaliyojengwa katika Shule za Msingi wilaya ya Singida na Ikungi. Shirika la WFP limetoa shilingi 95,271,600 kugharamia Ujenzi wa Matenki hayo.
 Kaimu mkuu wa wilaya ya Singida, Bura Gwando akizindua rasmi Matenki ya kuvunia Maji ya Mvua katika shule ya Msingi ya Igauri wilaya ya Singida. Kulia (mwenye shati jeusi) ni Meneja wa Shirika la SEMA, Ivo Manyaku. Shirika hilo ndilo lililojenga matenki hayo.
Moja ya tenki la kuvunia maji ya mvua lililopo katika shule ya msingi Igauri wilaya ya Singida.

Wednesday, September 4, 2013

Ama kweli Pombe si Chai!

 Vijana wawili wakazi wa manispaa ya Singida ambao hawakuweza kupatikana majina yao mara moja, wakiwa wamelala (saa nane mchana) kwa kile kilichodaiwa ni kutokana na kulewa kupitiliza. Wa kwanza kushoto inadaiwa awali alikuwa amelala juu ya bechi lakini alipozidiwa na usingizi, alidondoka chini na kuendelea kuuchapa usingizi. Katikati yao ni moja ya chupa ya pombe aina ya Banana waliyokuwa wanakunywa baada ya kumaliza viroba. Hivi karibuni kijana mmoja mkazi wa Kibaoni aliweza kuingiliwa kimwili kinyume na maumbile na rafiki yake,baada ya kulewa viroba kupindukia.

Ligi ya Mbunge wa jimbo la Singida Mjini “Mo Cup” yaanza kurindima mkoani Singida

Timu za za soka za kata ya Mitunduruni na Utemini zikiingia uwanjani namfua kufungua pazia la ligi ya kombe la mbunge wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Gullam Dewji (MO Cup).

Wachezaji wa timu za soka za kata ya Utemini na Mitunduruni manispaa ya Singida,wakisalimiana muda mfupi kabla hawajaanza mchezo wa fungua dimba wa ligi ya mbunge wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Gullam Dewji (MO Cup),kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida.

Wachezaji wa timu ya soka ya kata ya Utemini manispaa ya Singida,wakiwa kwenye picha ya pamoja muda mfupi kabla hawajaanza mchezo wa ligi ya kombe la MO dhidi ya kata ya Mitunduruni.

Wachezaji wa timu ya soka ya kata ya Mitunduruni manispaa ya Singida,wakiwa kwenye picha ya pomoja muda mfupi kabla hajaanza kucheza mechi ya ligi ya kombe la Mohammed Gullam Dewji,(MO Cup) dhidi ya timu ya soka ya kata ya Utemini.

Timu ya soka ya kata ya Utemini manispaa ya Singida,imeanza vema ligi ya kombe la mbunge wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Gullam Dewji (Kombe la MO), baada ya kuichapa kata ya Mitunduruni magoli 3-2.

Mchezo huo wa ufunguzi wa ligi ya kombe la MO, ulikuwa mkali na wa kusisimua na ulifanyika kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida. Mgeni rasmi alikuwa Katibu Uchumi wa CCM manispaa ya Singida, Mollel.

Timu hizo zilianza mchezo huo kila timu ikiusoma mchezo wa mpinzani wake.Kadri muda ulivyokuwa ukiongezaka, kila timu iliongeza mashambulizi kwa mpinzani wake.

Mitunduruni ndiyo iliyoanza kuzifumania nyavu za Utemini kupitia kwa Jumanne Ringi katika dakika ya 28.

Dakika sita baadaye Shii Shaban wa Utemini aliyeng’ara kwenye mechi hiyo,aliisawazishia timu yake kwa njia ya penalti.

Penalti hiyo ilitolewa na mwamuzi wa mchezo huo Anord Bungado baada ya

WATOTO NA PAKITI ZA VIROBA VYA POMBE KALI.

Watoto wakazi wa kata ya Ipembe manispaa ya Singida, wakichezea pakiti za viroba vya pombe kali aina mbalimbali vilivyonywewa na watumiaji kama walivyokutwa  na mpiga picha wetu. Pakaiti hizo za viroba ni hatari kwa Afya za Watoto hao endapo watamalizia akiba ya pombe kali inayobakishwa na wanywaji.

Sunday, September 1, 2013

Kijana wa kiume mkoani Singida aingiliwa kinyume na maumbile.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kijana mmoja mkazi wa Kibaoini Singida mjini, kulawitiwa na rafiki yake baada ya kulewa pombe ya viroba aina ya jogoo.

‘Ulevi noma’ hiyo imedhihirika baada vijana wawili wa kiume marafiki kunywa pombe nyingi na kuepelekea mmoja amwingilie kimwili kinyume na maumbile rafiki yake kipenzi.

Inadaiwa Athumani Juma mkazi wa Kibaoni alimwingilia kimwili kinyume na maumbile rafiki yake wa kiume mwenye umri wa miaka 26 (jina tunalo).

Kamanda wa polisi wa Singida ACP Geofrey Kamwela, amesema tukio hilo la aina yake, limetokea Agosti 27 mwaka huu saa tatu usiku eneo la soko la Kibaoni kata ya Kindai mjini Singida.

Amesema siku ya tukio, marafiki hao walikutana dukani ambapo mtuhumiwa Athumani alinunua viroba vinne aina ya jogoo, huku muathirika akinunua viroba tisa.

Kamanda Kamwela amesema baada ya kila mmoja kumaliza kunywa viroba vyake, muathirika alitangaza kuwa amelewa na hivyo kila mmoja arejee  nyumbani kwao.

Kamanda kamwela amesema “Walipofika eneo la soko la Kindai, muathirika alimwambia rafiki yake Athumani kuwa amwache hapo ili aweze kupumzika kwa vile pombe ilikuwa imemzidi sana, lakini ghafla..........

Halmashauri ya Singida yakusanya mapato ya zaidi ya shilingi bilioni 22 kutoka vyanzo yake mbalimbali.

 Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Singida Jumanne Mnyampanda (katikati) akiongoza kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha maendeleo ya wanancvhi mjini Singida. Wa kwanza kushoto ni makamu mwenyekiti halmashauri ya wilaya ya Singida Hamisi Mumbee na kulia ni Mkurugenzi wa halmashauri ya Singida Illuminata Mwenda.
 Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Singida wakifuatilia kwa makini hoja zilizokuwa zikijadiliwa kwenye kikao cha baraza la madiwani. Kikao hicho kilifanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha maendeleo ya wananchi mjini Singida.
Mwenyekiti wa huduma za jamii katika halmashauri ya wilaya ya Singida na diwani (CCM) wa kata ya Msange Elia Digha, akichangia hoja kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya Singida.

Halmashauri ya wilaya ya Singida imekusanya mapato kutoka vyanzo vyake mbalimbali zaidi ya shilingi bilioni 22.9 kati ya Julai mwaka jana na Juni mwaka huu.

Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Illuminata Mwenda amesema hayo wakati  akitoa taarifa yake ya mapato na matumizi kwenye kikao cha baraza la madiwani, kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha maendeleo ya wananchi mjini Singida.

 Amesema makusanyo hayo ya mapato ni sawa na asilimia 78 ya lengo la kukusanya shilingi 29,583,444,380 kwa mwaka huo wa fedha.

 Mwenda amesema kuwa vyanzo vya ndani vya mapato, walikusanya zaidi ya shilingi..........