Timu za za soka za kata ya Mitunduruni na Utemini zikiingia uwanjani namfua kufungua pazia la ligi ya kombe la mbunge wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Gullam Dewji (MO Cup).
Wachezaji wa timu za soka za kata ya Utemini na Mitunduruni manispaa ya Singida,wakisalimiana muda mfupi kabla hawajaanza mchezo wa fungua dimba wa ligi ya mbunge wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Gullam Dewji (MO Cup),kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida.
Wachezaji wa timu ya soka ya kata ya Utemini manispaa ya Singida,wakiwa kwenye picha ya pamoja muda mfupi kabla hawajaanza mchezo wa ligi ya kombe la MO dhidi ya kata ya Mitunduruni.
Wachezaji wa timu ya soka ya kata ya Mitunduruni manispaa ya Singida,wakiwa kwenye picha ya pomoja muda mfupi kabla hajaanza kucheza mechi ya ligi ya kombe la Mohammed Gullam Dewji,(MO Cup) dhidi ya timu ya soka ya kata ya Utemini.
Timu ya soka ya kata ya Utemini manispaa ya Singida,imeanza vema ligi ya kombe la mbunge wa jimbo la Singida mjini,Mohammed Gullam Dewji (Kombe la MO), baada ya kuichapa kata ya Mitunduruni magoli 3-2.
Mchezo huo wa ufunguzi wa ligi ya kombe la MO, ulikuwa mkali na wa kusisimua na ulifanyika kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida. Mgeni rasmi alikuwa Katibu Uchumi wa CCM manispaa ya Singida, Mollel.
Timu hizo zilianza mchezo huo kila timu ikiusoma mchezo wa mpinzani wake.Kadri muda ulivyokuwa ukiongezaka, kila timu iliongeza mashambulizi kwa mpinzani wake.
Mitunduruni ndiyo iliyoanza kuzifumania nyavu za Utemini kupitia kwa Jumanne Ringi katika dakika ya 28.
Dakika sita baadaye Shii Shaban wa Utemini aliyeng’ara kwenye mechi hiyo,aliisawazishia timu yake kwa njia ya penalti.
Penalti hiyo ilitolewa na mwamuzi wa mchezo huo Anord Bungado baada ya
Tamimu Ananas kuchezewa vibaya na Rinyo Salum.
Shafii aliifungia timu yake ya Utemini goli la pili katika dakika ya 40 baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa lango la Mitunduruni.
Zikiwa zimesalia dakika mbili kipindi cha kwanza kumalizika,Juma Idd aliisawazishia timu yake ya Mitunduruni baada ya kuifungia goli la pili.Hadi timu hizo zinaenda mapumzikoni, zilikuwa zimefungana goli 2-2.
Mchezaji mkongwe wa Utemini Ramadhani Ghuliko,aliihakikishia timu yake ushindi baada ya kuifungia goli la tatu katika dakika ya 88.
Jana ligi hilo ilitarajiwa kuendelea kati ya timu ya kata ya Majengo na Mughanga kwenye uwanja wa namfua.
No comments:
Post a Comment