Thursday, September 5, 2013

SEMA na WFP yakabidhi matenki ya kuvunia Maji ya Mvua kwa shule za msingi Sita mkoani Singida

 Meneja mkuu wa shirika la SEMA Ivo Manyaku, akitoa taarifa yake ya ujenzi wa matenki ya kuvunia Maji ya Mvua katika Shule Sita za Msingi za wilaya ya Singida na Ikungi. Matenki hayo yaliyogharimu zaidi ya shilingi 101.9,yanatarajiwa kupunguza kero ya Wanafunzi kupoteza muda mwingi wa masomo katika kutafuta maji.
 Mkuu wa ofisi ndogo ya mpango wa chakula Duniani (WFP) Dodoma, Nima Sitta akihimiza utunzaji wa Matenki ya kuvunia Maji ya Mvua yaliyojengwa katika Shule za Msingi wilaya ya Singida na Ikungi. Shirika la WFP limetoa shilingi 95,271,600 kugharamia Ujenzi wa Matenki hayo.
 Kaimu mkuu wa wilaya ya Singida, Bura Gwando akizindua rasmi Matenki ya kuvunia Maji ya Mvua katika shule ya Msingi ya Igauri wilaya ya Singida. Kulia (mwenye shati jeusi) ni Meneja wa Shirika la SEMA, Ivo Manyaku. Shirika hilo ndilo lililojenga matenki hayo.
Moja ya tenki la kuvunia maji ya mvua lililopo katika shule ya msingi Igauri wilaya ya Singida.

No comments:

Post a Comment