Monday, September 16, 2013

Mkuu wa mkoa wa Singida Amtembelea Hospitalini Mwandishi wa Mwananchi na The Citizen aliyekatwa Mapanga na Jambazi

 Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Vicent Kone akimjulia hali Mwandishi wa Habari wa Magazeti ya Mwananchi na The Citizen mkoa wa Singida, Awila Silla anayeendelea na matibabu katika hospitali ya mkoa mjini Singida, akitibiwa majeraha baada ya kukatwa katwa kichwani kwa Panga na kijana anayedaiwa kuwa ni Jambazi.


Mwandishi wa Habari wa Mwananchi na The Citizen Ajeruhiwa kwa Mapanga.


Mwandishi wa habari wa gazeti la The Citizen na mwananchi mkoani Singida, Awila Silla amenusurika kuuawa na mtu anadhaniwa kuwa Jambazi baada ya kukatwa katwa kichwani na kusababisha kuzirai. Tukio hilo limetokea juzi saa mbili usiku jirani na mahakama ya mwanzo ya Utemini mjini Singida. Awila ambaye amelazwa wodi 2  hospitali ya mkoa amedai baada ya kukutana na kijana huyo aliamuriwa

Thursday, September 12, 2013

KIJANA ADAIWA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA MJINI SINGIDA.



Vyandarua vyatumika kuezeka vyoo.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida Edward Ole Lenga akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kinampundu mara baada ya kukabidhiwa Zahanati na nyumba mbili za mganga na shirika moja lisilo la kiserikali la HAPA,hafla hiyo ilifanyikajuzi kijijini hapo.
 Ni Mwakilishi wa shirika la SIMAVI kutoka nchini Uholanzi Lieke Ongering akizungumza katika hafla ya kukabidhi mradi wake kwa ushirikiano na shirika la HAPA Singida kukamilisha mradi wa ujenzi wa Zahanati na nyumba mbili za mganga kijiji cha Kinampundu takribani umbali wa kilomita 70 kutoka mjini Singida.
Ni mmoja wa kinamama wajawazito akipimwa uzito na mkuu wa Wilaya ya Mkalama Ole Lenga mara baada ya kukabidhiwa vifaa vya zahanati hiyo, anayeshuhudia kipimo hicho ni mhasibu mkuu wa shirika hilo Noel Makyao.
Mkurugenzi wa HAPA Davd Mkanje  (Kulia) kimkabidhi DC wa Mkalama Ole Lenga baadhi ya vifaa vya kutolea huduma kwenye Zahanati hiyo wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya mradi huo.
Ni baadhi ya wageni kutoka Mataifa mbalimbali nje ya nchi wakicheza muziki na wananchi wa kijiji cha Kinampundu mara baada ya kukabidhiwa mradi huo wa afya ya uzazi wa mama na mtoto.
Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Ole Lenga, kushoto mwenye suti, mwakilishi wa SIMAVI, Lieke, MMkurugenzi wa shirika la HAPA, Davd Mkanje na mhasibu mkuu wa shirika hilo Noel Makyao wakifurahia pamoja na wananchi mara baada ya kukabidhi mradi huo.

Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida ameonya tabia ya baadhi wananchi kuezekea kwenye vyoo vyandarua vya kujikinga na mbu wa malaria.

Onyo hilo limetolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na Mkuu huyo wa Wilaya, Edward ole Lenga wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kinampundu muda mfupi baada ya kukabidhiwa Zahanti ya kijiji na shirika la HAPA.

Alisema imezuka tabia ya wananchi kutumia vyandarua hivyo kwa matumizi yasiyo rasmi ikiwa na pamoja na wengine kuvifanya kama mabanda ya kuhifadhi vifaranga vya kuku.

“Hii ni aibu, wenzetu wanatupatia vyandarua  ili tusipate malaria, nyie mnatumia kuezeka vyoo kwa kweli hii ni aibu kubwa sana na mimi nimetembea vijijini na kujionea hili, na kwa kweli atakayekamatwa atakiona cha moto.” Alisema Dc Lenga kwa masikitiko.

Aidha alisema serikali inatumia fedha nyingi kwa ajili ya kuagizi

Monday, September 9, 2013

Shirika lisilo la kiserikali lakabidhi Zahanati na Nyumba zenye thamani ya Tsh 115.9 mkoani Singida

 Mkurugenzi wa shirika la HAPA, David Mkanje akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya Zahanati na nyumba ya watumishi ya kijiji cha Kinampundu wilaya ya Mkalama. Kulia wa nne ni mkuu wa wilaya ya Mkalama na wa kwanza kushoto ni katibu tarafa Nduguti wilaya ya Mkalama, Nyalandu.
 Mkurugenzi wa shirika la HAPA,David Mkanje (kushoto) akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Mkalama, funguo za zahanati ya kijiji cha Kinampundu. HAPA imejenga zahanati hiyo na nyumba ya watumishi kwa gharama ya zaidi ya shilingi 115.9.
 Mkuu wa wilaya ya Mkalama,Edward Ole Lenga akifungua rasmi Zahanati ya kijiji cha Kinampundu.
Mkuu wa wilaya ya Mkalama mkoa wa Singida,Edward Ole Lenga akizungumza kwenye hafla ya kukabidhiwa zahanati ya kijiji cha Kinampundu.Wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa shirika la HAPA lililojenga zahanati hiyo kwa zaidi ya shilingi 115.9. Siku za nyuma wakazi zaidi ya 7,000 wa kijiji hicho, walikuwa wakitembea umbali wa zaidi ya kilomita 12 kufuata huduma ya afya.
Baadhi ya wageni kutoka Uholanzi, Amerika, Uingereza na Ireland waliohudhuria hafla ya makabidhiano ya zahanati na nyumba ya watumishi wa katika kijiji cha Kinampundu wilaya ya Mkalama.
Mkuu wa wilaya ya Mkalama Edward Ole Lenga akiwa na mwakilishi wa shirika la SIMAVI la nchini Uholanzi, Ljeke muda mfupi baada ya kuzindua nyumba ya watumishi wa zahanati ya kijiji cha Kinampundu.Wa pili kulia ni mkurugenzi wa shirika la HAPA, David Mkanje.

Shirika lisilo la kiserikali la Health Action Promotion Association (HAPA) la Mkoa wa Singida limetumia zaidi ya shilingi 115.9 milioni kugharamia ujenzi wa jengo la Zahanati na nyumba ya watumishi katika kijiji cha Kinampundu wilaya ya Mkalama.

Fedha hizo, pia zimetumika kununulia kitanda cha kuzalishia,vifaa vya kuzalishia, mizani ya watu wazima, mizani ya watoto wachanga, stendi ya drip na kitoroli cha kugawia dawa.

Hayo yamesemwa mwishoni mwa juma na Mkurugenzi wa HAPA, David Mkanje wakati akizungumza kwenye makabidhiano ya majengo hayo kwa uongozi wa wilaya ya Mkalama.

Alisema ujenzi wa jengo la zahanati pamoja na vyoo vyake, HAPA imetumia shilingi

Saturday, September 7, 2013

WFP watoa msaada wa pampu za maji zenye thamani Tsh 94 millioni mkoani Singida

Mkuu wa Ofisi ndogo ya Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Dodoma, Nima Sitta akihimiza utunzaji wa matenki ya kuvunia maji ya mvua yaliyojengwa katika shule za msingi wilaya ya Singida na Ikungi. Shirika la WFP limetoa shilingi 95,271,600 kugharamia ujenzi wa matenki hayo.

Shirika lisilo la kiserikali la Mpango wa chakula duniani (WFP) limetoa msaada wa pampu 210 za maji zenye thamani ya zaidi ya shilingi 94 milioni kwa shule za msingi na vikundi mbalimbali mkoani Singida.

Pampu hizo ni kwa ajili ya kilimo cha umwangiliaji bustani.

Hayo yamesemwa juzi na Mkuu wa Ofisi ndogo ya WFP Dodoma Nima Sitta,wakati akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya matenki 12 ya kuvunia maji ya mvua yaliyojengwa kwenye shule sita za wilaya ya Singida na wilaya ya Ikungi.Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya shule ya msingi Igaruri wilaya ya Singida.

Alisema lengo kuu la msaada huo wa pampu za maji,ni kila shule za msingi na vikundi vya vijana,kuanzisha

Friday, September 6, 2013

Wadau wa Ukimwi washauriwa kuongeza juhudi kwenye mapambano dhidi ya Ukimwi

 Afisa Ustawi wa Jamii katika Sekretarieti ya mkoa wa Singida, Zuhura Karya (kulia) akizungumza kwenye ufunguzi wa semina ya wadau wa vita dhidi ya UKIMWI wa wilaya ya Ikungi.Wa kwanza kushoto ni mratibu wa vita dhidi ya UKIMWI katika wilaya ya Ikungi, Mussa na wa pili kushoto ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi, Selestin Yunde. Semina hiyo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha maendeleo ya wananchi mjini Singida.
 Baadhi ya wadau wa vita dhidi ya UKIMWI wa wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida,wakifuatilia kwa makini semina ya siku moja iliyohusu kujadiliana na kuweka mikakati ya kumaliza kabisa maambukizi mapya ya VVU.Semina hiyo imefanyikia kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha maendeleo ya wananchi mjini Singida.

Wadau wa vita dhidi ya Ukimwi Wilayani Ikungi wametakiwa kutobweteka na kitendo cha kupungua kwa maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi na badala yake waongeze kazi ya kupambana na ugonjwa  huo ili ifikapo mwaka 2015 maambukizi, unyanyapaa na vifo vifikie asilimia sifuri.

Changamoto hiyo imetolewa juzi na Afisa Ustawi wa Jamii Sekretarieti ya Mkoa wa Singida,Zuhura Kyara,wakati akifungua mkutano wa wadau wa UKIMWI katika wilaya mpya ya Ikungi uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo Cha Maendeleo ya wananchi mjini hapa.

Alisema maambukizi mapya ya VVU katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida na Ikungi,takwimu zinaonyesha kuwa yamepungua kutoka asilimia nne hadi mbili mwaka huu.

Kyara alisema hayo ni mafanikio mazuri lakini hata hivyo,juhudi zaidi zinapaswa kuongezwa ili kufikia mwaka