Mwandishi wa habari wa gazeti la The Citizen na mwananchi mkoani Singida, Awila Silla amenusurika kuuawa na mtu anadhaniwa kuwa Jambazi baada ya kukatwa katwa kichwani na kusababisha kuzirai. Tukio hilo limetokea juzi saa mbili usiku jirani na mahakama ya mwanzo ya Utemini mjini Singida. Awila ambaye amelazwa wodi 2 hospitali ya mkoa amedai baada ya kukutana na kijana huyo aliamuriwa
kutoa Fedha na baada ya kudai hana, jibu hilo lilisababisha kijana huyo kuanza kumkata Mapanga na alipoangauka na kuzirai alinyang’anywa simu yake ya kiganjani .Hata hivyo Awila amedai kuwa bado hajatoa taarifa ya tukio hilo polisi.
E mungu nyosha mkono wako kwa mama yetu apone haraka awez kuendelea na majuku yake
ReplyDelete