Thursday, January 9, 2014

Manispaa ya Singida kuomba shilingi 3.5 bilioni Serikali kuu.

                           Mbunge wa Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji.

HALMASHAURI ya Manispaa ya Singida inatarajia kuwasilisha serikalini maombi maalum ya kuomba jumla ya shilingi 3.5 bilioni kwa ajili ya kugharamia maeneo manne ambayo ni ya kipaumbele katika mwaka wake wa fedha wa 2014/2015.

Hayo yamesemwa mwishoni mwa wiki na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida,Deus Lusiga wakati akiwasilisha mapendekezo ya bajeti ya mwaka ujao wa fedha mbele ya kikao maalum ya baraza la madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa manispaa hiyo.

Amesema Manispaa ya Singida imefikia uamuzi huo kutokana na ufinyu wa mapato na uwepo wa changamoto ya kujitosheleza katika mahitaji yake.

Lusiga alitaja vipaumbele hivyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa jengo jipya la Manispaa linalotarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi 2.7 bilioni.

Kaimu Mkurugenzi huyo alitaja vipaumbele vingine kuwa ni ununuzi wa gari na vifaa vya kuzolea taka ngumu na maji ambayo itagharimu 300 milioni,ujenzi wa madaraja,milioni 200 na ukamilishaji wa nyumba za walimu na madarasa katika shule za msingi ambapo zitatumika shilingi 300 milioni.

Kikao hicho kilichokuwa chini ya Mstahiki Meya,Sheikh Salum Mahami kwa kauli moja kimeazimia kwamba Mbunge wa Jimbo la Singida mjini,Mohammed Gullam Dewji asimamie maombi serikali ili matarajio yaweze kufikiwa.

Awali akifungua kikao hicho,Mstahiki Meya Sheikh Mahami alitumia fursa hiyo kuviomba vyombo vya habari kuitangaza vema na kwa usahihi bajeti hiyo ili

Mazingira ambayo mtoto wako anacheza kila siku, Je yako salama..???

Watoto wakazi wa kijiji cha Ilolo kata ya Mhintiri tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi, wakiogelea kwenye mto wa kijiji hicho kama walivyokutwa na mpiga picha wetu. Maji hayo licha ya kuwa ni machafu  mno, kuna uwezekano mkubwa watoto hao wakapata ugonjwa wa Kichocho.

Halmashauri ya Manispaa ya Singida kukusanya shilingi 31.7 bilioni 2014/2015.

Mstahiki meya wa manispaa ya Singida, Sheikh Salum Mahami,akifungua kikao maalum cha madiwani cha kupitisha mapendekezo ya bajeti ya mwaka ujao wa fedha.Kushoto ni naibu meya Hassan Mkata na kulia ni kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Singida na Afisa mipango,Deus Lusiga.
Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Singida, Deus Lusiga, akitoa ufafanuzi kwenye kikao maalum cha baraza la madiwani lililokuwa linapitisha mapendekezo ya bajeti 2014/2015.
Baadhi ya madiwani wa manispaa ya Singida,wakifuatilia kwa makini mapendekezo ya bajeti ya mwaka wa fedha wa 2014/2015.

HALMASHAURI ya Manispaa ya Singida inatarajia kukusanya mapato ya zaidi ya shilingi 31.7 bilioni kutoka vyanzo vyake mbalimbali vya mapato katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2014/2015.

Hayo yamesemwa hivi karibuni na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida,Deus Luziga wakati akitoa mapendekezo ya bajeti ya mwaka ujao wa fedha mbele ya kikao maalum cha madiwani kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa manispaa hiyo.

Luziga ambaye ni Afisa Mipango wa Manispaa ya Singida amesema wanatarajia kukusanya zaidi ya shilingi 2.9 biloni kutoka kwenye vyanzo vyake vya ndani.

Amesema wanatarajia serikali kuu itawapatia ruzuku ya shilingi 181,219,050 kwa ajili ya kufidia ushuru na kodi iliyofutwa.

“Serikali kuu pia tunatarajia itatupa zaidi ya shilingi 15.2 bilioni kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa umma,itatupatia pia ruzuku ya zaidi ya shilingi 1.8 bilioni ya matumzi yasiyo ya mishahara na ruzuku ya miradi ya maendeleo ya zaidi ya shilingi 11.6 bilioni’,amesema.

Kaimu Mkurugenzi huyo amesema bajeti ya Manispaa ya Singida imeongezeka kwa shilingi 13,630,476,230 ambayo ni sawa na asilimia 43 ya lengo la kukusanya zaidi ya shilingi 18.1 bilioni katika bajeti ya mwaka wa fedha wa 2013/2014.

“Ongezeko hili limechangiwa pamoja na kuongezeka kwa ajira mpya na nyongeza za mishahara na kuongezeka kwa

Wakazi wa kijiji alikozaliwa IGP Mangu wapokea uteuzi wa mwana wao kwa bashasha.

Mama mzazi wa IGP Ernest Mangu,mkazi wa kijiji cha Kihanuda tarafa ya Ilongero wilaya ya Singida, Bi. Mwanaidi Msengi akipasua kuni  kwa ajili ya kupikia chakula.
Mama mzazi wa IGP, Ernest Mangumkazi wa kijiji cha Kihanuda tarafa ya Ilongero wilaya ya Singida,akiwa amejitwisha chungu akiwa nyumbani kwake.Mama huyo,amedai kuwa alifanya biashara ya kuuza vyumba na kupata fedha za kugharamia masomo ya Mangu.
Makazi ya wazazi wa IGP Ernest Mangu yaliyoko katika kijiji cha Kihanuda tarafa ya Ilongero wilaya ya Singida.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam.

UTEUZI  wa Mkuu Mpya wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Kamishna Ernest Mangu umepokelewa kwa nderemo, vifijo na bashasha na wakazi wa kijiji cha Kihunadi tarafa ya Ilongero wilaya na mkoa wa Singida alikozaliwa IGP huyo kwa madai kwamba sasa kijiji chao kitajulikana haraka ndani na nje ya Tanzania.

Wamedai pamoja na faida ya kujulikana huko,changamoto mbali zinazokikabili kijiji hicho zitapatiwa ufumbuzi wa kudumu mapema iwezekanavyo.

Wamedai zaidi kwamba wamekuwa wakiamini kwa Kamishna Mangu atafika mbali katika kushika nafasi za juu za uongozi kutokana na uadilifu, uchapaji kazi, ukaribu wake kwa wananchi, uaminifu na uwazi wake.

Kwa upande wa mama yake mzazi Mwanaidi Msengi, pamoja na furaha kubwa aliyonayo, amemwasa mtoto wake huyo kuchapa kazi kwa bidii kama njia mojawapo ya kumshukuru Rais Kikwete kwa kumteua kuwa mzawa wa kwanza wa mkoa wa Singida, kushika wadhifa huo nyeti.

“Hii ni heshima kubwa sana kwangu binafsi, ndugu zake, wakazi wa kijiji cha Kihunadi na mkoa wa Singida, kwa hiyo lengo langu ni kumwombea mtoto wangu Mangu asimwangushe Rais, atimize wajibu wake ipasavyo ili Rais Kikwete siku moja aseme hajakosea kumpa Mangu, ukuu wa polisi nchini”,amesema kwa kujiamini.

Mwanaidi amesema Mangu alianza elimu ya msingi katika shule ya Kinyagigi, alikuwa na bidii mno katika kujisomea.  Kwenye mitihani mara nyingi alishika nafasi ya kwanza au  ya pili, akifanya vibaya alishika nafasi ya tatu.

“Mwaka 1977 alifaulu mtihani wa darasa la saba na kuchaguliwa kujiunga na elimu ya sekondari katika shule ya Tumaini iliyopo Kinampanda wilayani Iramba aliyomaliza kidato cha nne”,amesema.

Akifafanua, Mwanaidi amesema alipofaulu kujiunga na elimu ya sekondari, alilazimika kuomba ng’ombe kwa mke mweza, ili akamuuze apate fedha za kugharamia masomo ya mtoto wake.

“Nadhani mke mwenzangu huyo, alimtoa ng’ombe wake kwa shingo upande kwa sababu Mangu alipomuuza kwenye mnada pale Singida mjini, aliibiwa fedha zote na alirudi nyumbani akilia sana”,amesema.

Amesema baada ya hapo, alimwambia mtoto wake Mangu, kwamba hawataomba tena ng’ombe na badala yake atatengeneza vyungu kwa kutumia udongo wa mfinyanzi  ili kupata fedha za kugharamia masomo yake.

“Nashukuru Mangu alinielewa vizuri kwa sababu alishiriki kubeba kichwani vyungu hivyo wakati wa kuviuza hadi kichwa chake kilikaribia kuwa kipara.  Nilibuni chanzo kingine cha mapato ambacho kilikuwa ni kukoroga na kuuza

Wakala wa M-pesa ajipiga risasi kichwani na kufa papo hapo.

Baadhi ya wakazi wa mjini Singida, wakiwa wamekusanyika katika duka la wakala wa M-pesa lililopo kwenye taasisi ya elimu ya watu wazima, muda mfupi baada ya mmiliki wa duka hilo Mashaka Omari Makiya,kujipiga risasi kwa kutumia Bastola yake na kusababisha kifo chake.
Mwandishi wa habari wa radio na TV Clouds mkoani Singida, John,akisoma wosia (haupo kwenye picha)  ulioachwa na mfanyabiashara Mashaka Omari Makiya,aliyejiua kwa kujipiga risasi kwa bastola yake.Wosia huo umedai kuwa wadogo wa marehemu wakabidhiwe nyumba na fedha alizoziacha.

WAKALA Maarufa wa M-pesa Vodacom na Mkazi wa Kibaoni mjini Singida Mashaka Omari Makiya (30) amejipiga risasi kichwani na kusababisha kifo chake papo hapo.

Mashaka maarufu kwa jina la Mashakom, amejipiga risasi kwa kutumia bastola yake aina ya ‘silencer’ usiku wa Desemba 27 mwaka huu, nyumbani kwake Ipembe mjini hapa.

Shuhuda wa tukio hilo,Shija John amesema Desemba 28 mwaka huu saa saba mchana askari polisi walifika nyumbani kwa marehemu iliyopo mkabala na nyumba ya kulala wageni ya Meatu eneo la Ipembe.

Amesema askari polisi hao waliingia chumbani kwa Mashaka ambapo walikuta mwili wa mfanyabiashara huyo ukiwa sakafuni.Pia walikuta bastola yake ikiwa pembeni mwa mwili huo pamoja na simu zake tatu.

“Taarifa nilizonazo ni kwamba mfanyakazi wa Mashaka aligundua tukio hilo na kisha alitoa taarifa kituo kikuu cha kati cha polisi na askari walifika mara moja”,amesema.

Katika hatua nyingine, mwandishi wa habari hizi aliweza kufika kwenye moja ya maduka yake matatu ya M-pesa na kushuhudia ujumbe wa maandishi ulioachwa na Mashaka ndani ya gari lake jeusi.

Pamoja na askari polisi kukataa kutoa kibali kwa waandishi habari  kusoma ujumbe huo au kuupiga picha,watu waliobahatika kuusoma ukiwa ndani ya gari wamedai kuwa marehemu amemhusisha na kifo chake mfanyabiashara mmoja (jina tunalo) aliyekuwa na mahusiano ya karibu ya kibiashara pia marehemu Mashaka ameagiza kuwa nyumba na fedha zake wapewe wadogo zake.

Kifo cha Mashaka kimezua hofu kubwa na kazi ya uwakala wa M-pesa kwa madai kwamba katika miaka michache waliokuwa wafanyabiasha wa uwakala huo,Tembs na Rweyemamu wote wamepoteza maisha kwa kupigwa risasi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela amesema

Wednesday, January 8, 2014

Halmashauri ya Ikungi kutumia shilling 512.3milioni kwenye miradi ya maendeleo.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ikungi, Protace Magayaye, akitoa taarifa yake kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha)  ya utekelezaji wa shughuli za kilimo msimu wa 2013/2014 ambapo wanatarajia kuvuna tani 144,826 mazao ya chakula na hivyo kuwa na ziada tani 83,090.Mahitaji ya wakazi wa wilaya hiyo 225,521,ni tani 61,736 kwa mwaka.

HALMASHAURI ya Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida inatarajia kutumia zaidi ya shilingi 512.3 milioni kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ya wananchi katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2013/2014.
Fedha hizo zimepokelewa na Halmashauri hiyo hadi kufikia mwezi huu wa Desemba mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Protace Magayane wakati akizungumza na moja ya magazeti ya kila siku ofisini kwake juu ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi.
Alitaja baadhi ya miradi ya maendeleo wanayoitekeleza kuwa ni ujenzi wa hostel katika shule ya sekondari Ikungi ujenzi wa nyumba ya watumishi ya kijiji cha Kimbwi na kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto wenye mahitaji maalum wa shule ya msingi Ikungi.

Magayane alitaja miradi mingine kuwa ni kuendesha mafunzo ya mashamba darasani kwa wakulima 10 na ununuzi wa mbegu bora, ukarabati wa tanki la maji Iyumbu na matengenezo ya barabara za vijiji vya Mungaa-Ntuntu,Utaho-Makiungu na Ikungi- Ndung’unyi.
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi huyo alitaja baadhi ya mikakati ya kuboresha utekelezaji miradi kuwa ni uongozi wa Halmashauri kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo kuendelea kuzihamasisha jamii kushiriki kuchangia, kutunza na kumiliki miradi yao.

“Kuhakikisha vijiji na kata zinatoa taarifa za

Waandishi wa Habari wa Singida wahimizwa kujitathimini kwenye utendaji wao wa kazi.

Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida,Yahaya Nawanda, akifungua mkutano wa wadau wa habari na wanachama wa klabu ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida  uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya ya Iramba.
Baadhi ya wanachama wa klabu ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida,wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zinatolewa kwenye mkutano wa wadau wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya ya Iramba.

WAANDISHI wa Habari mkoani Singida wamehimizwa kufanya tathimini ya kina juu ya utendaji wao wote wa mwaka huu ili kujijengea mazingira mazuri zaidi ya utendaji wao katika kipindi cha mwaka ujao.

 Changamoto hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoa wa Singida,Yahaya Nawanda wakati akifungua mkutano wa pamoja kati ya wadau wa habari na wanachama wa klabu ya Waandishi wa Habari (Singpress) Mkoa wa Singida.

Amesema utamaduni wa mtu kujikagua na kujitathimini mara kwa mara,kunachochea mhusika kuboresha utendaji wake na hivyo kwa kiasi kikubwa kujiletea maendeleo endelevu.

 “Usipojitathimini,utadumaza utendaji wako au utashindwa kuboresha maisha/maendeleo na kwa kiasi kikubwa maendeleo yako yataporomoka kwa kasim kubwa”,alifafanua Nawanda.

 Akifafanua zaidi,mkuu huyo wa wilaya,alisema mwandishi wa habari anapaswa kujiuliza mwaka huu,ameandika habari zipi na ipi imemletea mafanikio zaidi,ili mwakani aweze kuja na mbinu mpya zaidi na mikakati itakayomsaidia kupiga hatua zaidi.

 Aidha,Nawanda aliwataka wawe wabunifu na wajenge utamaduni wa kufanya tafiti za kina zitakazowasaidia kuibuka na stori zenye ubora wa hali ya juu.

 “Mwandishi wa habari acheni tabia ya kusubiri kuletewa habari,fanyeni tafiti za kina katika masuala ya kijamii utamaduni na kiuchumi Kwa njia hiyo mtakuwa waandishi wa habari wa viwango vya juu”,amesema.

 Katika hatua nyingine,Nawanda aliwaasa