Wednesday, January 8, 2014

Waandishi wa Habari wa Singida wahimizwa kujitathimini kwenye utendaji wao wa kazi.

Mkuu wa wilaya ya Iramba mkoa wa Singida,Yahaya Nawanda, akifungua mkutano wa wadau wa habari na wanachama wa klabu ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida  uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya ya Iramba.
Baadhi ya wanachama wa klabu ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida,wakifuatilia kwa makini mada zilizokuwa zinatolewa kwenye mkutano wa wadau wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya ya Iramba.

WAANDISHI wa Habari mkoani Singida wamehimizwa kufanya tathimini ya kina juu ya utendaji wao wote wa mwaka huu ili kujijengea mazingira mazuri zaidi ya utendaji wao katika kipindi cha mwaka ujao.

 Changamoto hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mkoa wa Singida,Yahaya Nawanda wakati akifungua mkutano wa pamoja kati ya wadau wa habari na wanachama wa klabu ya Waandishi wa Habari (Singpress) Mkoa wa Singida.

Amesema utamaduni wa mtu kujikagua na kujitathimini mara kwa mara,kunachochea mhusika kuboresha utendaji wake na hivyo kwa kiasi kikubwa kujiletea maendeleo endelevu.

 “Usipojitathimini,utadumaza utendaji wako au utashindwa kuboresha maisha/maendeleo na kwa kiasi kikubwa maendeleo yako yataporomoka kwa kasim kubwa”,alifafanua Nawanda.

 Akifafanua zaidi,mkuu huyo wa wilaya,alisema mwandishi wa habari anapaswa kujiuliza mwaka huu,ameandika habari zipi na ipi imemletea mafanikio zaidi,ili mwakani aweze kuja na mbinu mpya zaidi na mikakati itakayomsaidia kupiga hatua zaidi.

 Aidha,Nawanda aliwataka wawe wabunifu na wajenge utamaduni wa kufanya tafiti za kina zitakazowasaidia kuibuka na stori zenye ubora wa hali ya juu.

 “Mwandishi wa habari acheni tabia ya kusubiri kuletewa habari,fanyeni tafiti za kina katika masuala ya kijamii utamaduni na kiuchumi Kwa njia hiyo mtakuwa waandishi wa habari wa viwango vya juu”,amesema.

 Katika hatua nyingine,Nawanda aliwaasa

wadau wa habari kuendelea kushirikiana na Waandishi wa Habari Wakati huo huo,ni lazima mtambue kuwa mwandishi wa habari ni binadamu kama binadamu wengine,akiteleza,ifahamike sio kwa makusudi.

No comments:

Post a Comment