Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Kassim Majaliwa
(Mb), akizungumza na walimu wakuu wa shule za sekondari mkoa wa Singida
na baadhi ya watendaji wa sekta ya elimu. Mazungumzo hayo ambayo
yalikuwa ni pamoja na kuweka mikakati ya kuinua taaluma mkoani Singida
yamefanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa mjini
Singida. Kushoto ni kaimu mkuu wa mkoa wa Singida ambaye pia ni mkuu wa
wilaya ya Ikungi, Manju Msambya na Kulia ni katibu tawala mkoa wa
Singida, Liana Hassan.
Baadhi ya walimu wakuu wa shule za sekondari mkoa wa Singida wakimsikiliza kwa makini Mh. Kassim Majaliwa (hayupo kwenye picha).
Baadhi ya walimu wakuu wa shule za sekondari mkoa wa Singida wakimsikiliza kwa makini Mh. Kassim Majaliwa (hayupo kwenye picha).
Naibu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa Mhe. Kassim Majaliwa, amesema kuanzia sasa kazi ya kuandikisha
wanafunzi kuanza madarasa ya awali na yale ya msingi, itafanywa na
watendaji wa vijiji na si walimu wakuu wa shule za msingi.
Majaliwa
amesema hayo wakati akizungumza na walimu wakuu wa shule za sekondari
na baadhi ya viongozi wa sekta ya elimu mkoani Singida.
Amesema
kutokana na