Friday, February 15, 2013

Matembezi ya mshikamano katika kuadhimisha miaka 36 ya kuzaliwa CCM yafana mkoa wa Singida

 Makamu wa pili wa rais Zanzibar na mlezi wa CCM mkoa wa Singida, Balozi Seif Idd (mwenye kofia) akishiriki matembezi ya mshikamano ya CCM mkoa wa Singida,yaliyofanyika leo kama sehemu ya maadhimisho ya CCM kutimiza miaka 36 toka kianzishwe.Mwenye bukta ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindai na wa pili kulia ni mke wa balozi Seif.
 Mlezi wa CCM mkoa wa Singida, Balozi Seif Idd (wa tatu kushoto) akishiriki matembezi ya CCM ya  kilometa tano ya mshikamano yaliyofanyika mjini Singida leo.Mwenye truck suit ya blue ni mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone na wa pili kulia ni mke wa Balosi Seif Idd.Wa pili kushoto ni mbunge wa jimbo la Manyoni mashariki, John Chiligati.
 Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko  Kone,( wa tatu kulia) akishiriki matembezi ya mshikamano ya CCM yakiwa ni sehemu ya maadhimisho ya CCM kutimiza miaka 36 toka kizaliwe.Wa pili kulia ni MNEC manispaa ya Singida, Hassan Mazala.Wa kwanza kulia ni mkuu wa wilaya ya Mkalama, Edwerd Ole Lenga na anayefuatia ni mbunge wa jimbo la Manyoni mashariki, John Chiligati.
 Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone (mwenye truck suit ya blue) akiongoza wanaCCM kufanya mchakamchaka kwenye matembezi ya mshikamano ya CCM mkoa wa Singida.
 Katibu wa CCM mkoa wa Singida, Naomi Kapambala ( wa mbele) akiongoza kuimba nyimbo za uhamasishaji kwa wanaCCM walioshiriki matembezi ya mshikamano mbele ya ofisi ya CCM mkoa wa Singida.

No comments:

Post a Comment