Friday, February 15, 2013

Kutoweka kwa mashahidi wa mashitaka kesi inayowakabili vigogo wa CHADEMA Singida kwasababisha kesi kuahirishwa

 Mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya kumtolea lugha ya matusi mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi Mwita Waitara Mwakibe akitoka nje ya mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida baada ya kesi yao kuahirishwa leo, Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 11 mwaka huu,baada ya mashahidi wa upande wa mashitaka kuingia mitini.
Wakili wa washitakiwa vigogo wa CHADEMA Onesmo Kyauke (katikati) akiwaeleza jambo wateja wake muda mfupi baada kesi ya wateja wake kuahirishwa hadi Machi 11 mwaka huu.Vigogo hao wanaoshitakiwa kwa kumtolea
lugha ya matusi mbunge wa jimbo la Iramba magharibi, Mwigullu Lameck Nchemba.  Dk.Kitila Mkumbo (kushoto) na afisa sera na utafiti, Mwita Waitara Mwakibe (kulia).

No comments:

Post a Comment