Mbunge
wa jimbo la Singida mjini Mh. Mohammed Gullam Dewji akizungumza na
mmoja kati ya walemavu watano aliowakabidhi baiskeli za magurudumu
matatu kwa ajili ya kuwasaidia kumudu maisha yao hivi karibuni.Pamoja na
msaada wa baiskeli hizo, Dewji pia alitoa msaada wa Wheel Chair 24 kwa
hospitali ya rufaa ya mkoa wa Singida.Thamani ya msaada huo ni zaidi ya
shilingi milioni 14.
Mbunge
wa jimbo la Singida mjini, Mohammed Gullam Dewji ametoa msaada wa viti
24 maalum vya wagonjwa (wheel chairs) vyenye thamani ya zaidi ya
shilingi 24 milioni, kwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Singida.
Pamoja na viti hivyo mbunge huyo ametoa msaada wa baiskeli za magurudumu matatu kwa walemavu watano wa jimboni kwake.
Akizungumza
kwenye makabidhiano ya msaada huo, Dewji amesema msaada huo ni
mwendelezo wa misaada mbalimbali anayoitoa jimboni kwake, kwa ajili ya
kusaidiana na serikali kuboresha huduma mbalimbali zikiwemo za sekta ya
afya.
Alisema ana aimani kwamba
viti hivyo vitasaidia wagonjwa katika hospitali hiyo hasa wale watakaokuwa hawawezi kutembea.
“Tunaochoomba tu ni kwamba viti hivi vitunzwe vizuri ili viweze kutumika kwa muda mrefu”,alisema mbunge huyo.
Awali
mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa, Dk.Suleiman Muttani amepongeza
mbunge Dewji kwa msaada huo ambao amedai umekuja kwa wakati muafaka.
Dk.Muttani
amesema hospitali hiyo inayoendelea kujengwa ina mahitaji mengi na
makubwa yakiwemo ya vitendea kazi ambavyo serikali ikiachiwa ifanye peke
yake, itachukua muda mrefu kukidhi mahitaji ya hospitali hiyo ambayo
itategemewa pia na mikoa jirani.
“Kwa
kweli nakushukuru sana mbunge wetu kwa msaada huu wa viti.Tunakuomba
usichoke kuisaidia vifaa hii hospitali ya rufaa.Tusaidie pia
kuwahamasisha marafiki zako au taasisi mbalimbali ziweze/waweze
kutusaidia vitendea kazi kwa kadri ya uwezo wao”,amesema Dk.Muttani.
Kwa
mujibu wa Dk.Muttani, hospitali hiyo ya rufaa itakapokamilika itakuwa
na majengo 47 yenye thamani ya zaidi ya shilingi 150 bilioni.
Serikali
kila mwaka imekuwa ikitenga shilingi bilioni mbili kwa ajili ya
ujenzi.Kwa utaratibu huo wa kutenga kiasi hicho cha fedha hospitali hiyo
itachukua zaidi ya miaka 45 kukamilika kujengwa.
No comments:
Post a Comment