Thursday, February 21, 2013

Polisi mkoani Singida yakamata kilo 10.5 za Bangi na watuhumiwa wawili watiwa mbaroni.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP, Linus Sinzumwa.

Jeshi la polisi mkoa wa Singida limefanikiwa kukamata bunda 30 na misokoto 3,000 ya madawa ya kulevya aina ya bangi ambayo ni sawa na kilo 10.5.
Akizungumza na Singida Yetu Blog kwa njia ya simu, Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP Linus Sinzumwa, amesema kuwa bangi hiyo imekamatwa Februari 16 mwaka huu saa saba mchana ikiwa imehifadhiwa nyumbani kwa Williamu Kajuna (43) mkazi wa maeneo ya Mwenge mjini Singida.
Amesema kuwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa
raia wema, walifanya upekuzi katika nyumba ya William na kufanikiwa kukamata madawa hayo ya kulevya yakiwa yamefichwa chumbani chini ya ndizi mbichi kwa lengo la kuficha harufu kali ya madawa hayo.
Kamanda Sinzumwa ametumia fursa hiyo kuwashukuru na kuwapongeza wananchi wema kwa kulisadia jeshi la polisi taarifa sahihi iliyopelekea kukamatwa kwa William Kajuna na Msafiri Jackson (33) na kuwataka waendelee na moyo huo huo ili kutokomeza kila aina ya uhalifu mkoani hapa.
 Aidha, aliwataka madereva wa magari ya kusafirishia abiria kulisaidia jeshi la polisi katika kuwafichua watu wanaojihusisha na usafirishaji wa madawa ya kulevya yakiwemo mirungi na bangi.

No comments:

Post a Comment