Friday, February 15, 2013

Mkuu wa mkoa wa Singida aagiza waalimu wakuu wakajifunze matumizi ya fedha kwa mwalimu mkuu mwenzao

 Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Kone akizungumza na baadhi ya walimu wa shule ya sekondari Mwanzi Manyoni mjini.Dk.Kone hakufurahishwa na hali duni ya ofisi ya mkuu wa shule hiyo wakati shule ikiwa na akiba ya zaidi ya shilingi milioni sita.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi mchanganyiko Ikungi wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Olivary Kamili akiwa ofisini kwake akitekeleza majukumu yake. Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Kone ameagiza walimu wakuu wa shule za msingi na wakuu wa sekondari wafike shule ya msingi mchanganyiko Ikungi, ili wakajifunze juu ya matumizi bora ya fedha za Umma.

No comments:

Post a Comment