Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone, akizindua utoaji wa chanjo kimkoa katika hospitali ya St.Calorus iliyopo kijiji cha Mtinko. Jumla ya watoto 3,999 wanatarajiwa kupatiwa chanjo mbalimbali.
Mkuu wa mkoa wa Singida, Dk.Parseko Kone, akizungumza na wakazi wa tarafa ya Mtinko wilaya ya Singida, muda mfupi baada ya kuzindua zoezi la chanjo kimkoa lililoanza jana na linatarajiwa kumalizika Aprili 30 mwaka huu.
JUMLA ya watoto 3,999 mkoani Singida wanaositahili kupata chanjo mbalimbali,wanatarajiwa kupatiwa chanjo katika kipindi cha wiki ya chanjo iliyoanza aprili 24 hadi 30 mwaka huu.
Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone, wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa wiki ya chanjo kitaifa ngazi ya kimkoa uliofanyika katika hospitali ya St.Calorus kijiji cha Mtinko.
Mkuu huyo wa mkoa,amesisitiza kuwa ni muhimu sana kuhakikisha kila mtoto,anapata chanjo zote kwa wakati,ili kukidhibiti milipuko ya magonjwa mbalimbali.
“Magonjwa yanayolengwa na mpango wa chanjo wa taifa,ni kifua kikuu,donda koo,kifaduro,polio,surua,pepo punda,homa ya ini,homa ya uti wa mgongo,kichomi na kuhara”,alifafanua.
Dk.Kone alisema ili lengo la utoaji chano hizo liweze kufikiwa, ni lazima wataalam,wasimamizi wa chanjo wabadilike kwa kubuni mbinu mpya za kuhamasisha wananchi kuwapeleka watoto wote wanaostahili kupatiwa chanjo mbalimbali kwenye vituo vya kutolea huduma.
“Kwa ujumla,kila mmoja wetu anawajibu wa kuhakikisha