Meneja Mawsiliano TRCA, Bw. Innocent Mungy.
WAKAZI wa Manispaa ya Singida wameshauriwa kununua ving’amuzi kwa wakala walioteuliwa na mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), ili kuondoa uwezekano wa kupoteza fedha zao kwa kununua ving’amuzi ‘feki’.
Tahadhari hiyo imetolewa hivi karibuni na Meneja Mawsiliano TRCA, Innocent Mungy, wakati akizungumzia uzimaji wa mitambo ya kurusha matangazo ya televisheni ya mfumo wa utangazaji wa analojia utakaofanyika Singida Machi 31 mwaka huu saa sita usiku.
Amesema mawakala walioteuliwa na TRCA kuuza ving’amuzi Singida,kwa sasa wana ving’amuzi vya kutosha kukidhi mahitaji yaliyopo.
Alitaja mawakala hao kuwa ni Mushi Original, Saimon Malya, Baltazar Mushi (ana maduka mawili), Kweka Elextronic na Msele.
“Kwa hiyo kila mwenye hitaji la king’amuzi,ahakikishe ananunua kwenye maduka ya mawakala wetu,watakaonunua nje ya maduka hayo kuna uwezekano mkubwa wakanunua ving’amuzi vyenye
kiwango cha chini”,alifafanua.
Aidha,Mungy amesema mafundi watakaofunga ving’amuzi hivyo wanapatikana kwa wakala wa TCRA.
Katika hatua nyingine,amesema maandalizi ya kuzima mitambo ya analojia ya utangazaji wa televisheni kwa Singida na Tabora yamekamilika.
Mungy amesema vigezo vinavyotumika kuzima mitambo ya Analojia,ni pamoja na kuwepo utangazaji wa mfumo wa Analojia pamoja na kidijitali kwenye eneo husika, uapatikanaji ving’amuzi na uwepo wa chanel tano za kitaifa kwenye mfumo wa kidijiti.
No comments:
Post a Comment