Naibu Waziri wa Fedha na Mbunge wa jimbo la Iramba magharibi, Mh. Mwigulu Nchemba akihutubia wapiga kura wake na wananchi wa kata ya Mtoa tarafa ya Shelui ambapo pamoja na mambo mengine, alihimiza ujenzi wa zahanati kwa kila kijiji.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Kebwe Stephen Kebwe (MB) akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mgongo tarafa ya Shelui jimbo la Iramba magharibi ambapo amewataka Wakurugenzi wa halmashauri za majiji, manispaa na wilaya kuhakikisha magari ya kubebea wagonjwa hayatumiki kusafirisha bidhaa yoyote ikiwemo mkaa.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Kyengenge jimbo la Iramba magharibi, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Kebwe Stephen Kebwe (hayupo kwenye picha) ambaye aliwataka waganga wakuu wa halmashauri za majiji, manispaa na wilaya, kusimamia kikamilifu matumizi ya dawa na vitendea kazi.
Ambulince T.821 CUV iliyotolewa msaada na mbunge wa jimbo la Iramba magharibi, Mh. Mwigullu Nchemba kwa wakazi wa tarafa ya Shelui.Ambulance hiyo imemgharimu Mwingullu zaidi ya shilingi 50 milioni.

Mbunge wa jimbo la Iramba magharibi, Mh. Mwigullu Nchemba akisalimiana na timu ya soka ya kijiji cha Kyengenge.
SERIKALI imewaonya wakurugenzi wa halmashauri za majiji, manispaa na wilaya nchini, kuhakikisha wanasimamia kikamilifu matumizi sahihi ya magari ya kubebea wagonjwa (Ambulance), vinginevyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Onyo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Kebwe Stephen Kebwe (Mb), wakati akizungumza kwenye hafla iliyofana ya kukabidhi msaada wa gari la kubebea wagonjwa (Ambulance), lililotolewa na mbunge wa jimbo la Iramba magharibi, Mwigulu Nchemba kwa wakazi wa tarafa ya Shelui.
Alisema mfanyakazi/dereva akibainika amebadilisha matumizi ya magari hayo ya kubebea wagonjwa na kuanza kubeba mikaa, abiria au nafaka, ahesabu moja kwa moja kwamba, amejifukuza kazi.
“Mkurugenzi wa halmashauri husika naye akibainika kutowajibika kikamilifu kuhusu kusimamia magari hayo yanatumika kwa lengo la kusafirisha wagonjwa tu, nao watachukuliwa hatu akali za kisheria”,alisisitiza Dk.Kebwe.
Aidha, Dk. Kebwe ambaye pia ni mbunge (CCM) wa jimbo la Sengerema, amewaasa waganga wakuu wa halmashauri za majiji, Manispaa na wilaya, kusimamia vizuri i matumizi ya madawa na vitendea kazi, ili huduma za afya ziweze kukidhi mahitaji ya wananchi.
“Mganga mkuu ye yote katika halmashauri atakayebainika kuzembea au kuruhusu wizi wa dawa/vitendea kazi, atakuwa amepoteza sifa yake ya uganga mkuu na hivyo italazimika kuchukuliwa hatua za ksiheria”,alisema.
Katika hatua nyingine,Dk. Kebwe amewataka wananchi
kuendelea na moyo wao wa kuchangia maendeleo yao ikiwemo ujenzi wa nyumba za watumishi wa afya.
“Wananchi wanalojukumu kubwa la kuchangia maeneleo yao ikiwemo kuhakikisha vituo vya afya vinakuwa na nyumba za kutosha za kuishi watumishi.Bila nyumba za kutosha kwa watumishi wentu wa sekta ya afya,tutakuwa tumetoa mwanya watumishi kuweza kutukimbia”,alisema.
Wakati huo huo, naibu waziri huyo alitumia fursa hiyo kumpongeza Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, kwa juhudi zake za kuwaondolea kero wananchi wa jimbo lake ikiwemo kuwapa msaada wa Ambulance ambalo litawasaidia hasa akina mama wajawazito kuwahi kwenye vituo vya afya.
No comments:
Post a Comment