Sunday, May 4, 2014

Dkt. Kone awahimiza Wanafunzi kusoma masomo ya Sayansi.

Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Vicent Kone, akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani (mei mosi),yaliyofanyika kimkoa katika uwanja wa namfua mjini Singida (01/5/2014).Maadhimisho ya mwaka huu kwa mkoa wa Singida yalihudhuriwa na watumishi wa umma na wananchi wachache ukilinganisha na miaka iliyopita.Kushoto ni mratibu wa RAAWU mkoa wa Singida na mwenyekiti wa kilele cha maadhimisho ya  sherehe ya siku kuu ya wafanyakazi duniani (Mei mosi mwaka huu).
Mkuu wa mkoa wa Singida Dk.Parseko Vicent Kone.(wa tatu kulia) akishiriki kuimba wito wa mshikamano wa wafanyakazi.Wa kwanza kulia ni Misholi (wa pili kulia) ni Blandina Marwa wenyekiti wa sherehe za mei mosi mkoa wa Singida na mratibu wa RAAWU mkoani Singida.
Mkuu wa mkoa wa Singida,Dk.Parseko Kone, akimkabidhi cheti mfanyakazi bora wa mwaka huu wa TANESCO mkoani Singida ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani – Mei Mosi.Pamoja na cheti, mfanyakazi huyo Ps wa menejaTANESCO makao makuu mkoani Singida, pia alizawadiwa Tv screen yenye thamani ya shilingi laki nane.
Baadhi ya viongozi na watendaji wa serikali waliohudhuria kilele cha maadhimisho ya wafanyakazi duniani yaliyofanyika kimkoa kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida.Mwenye miwani ni hakimu mfawidhi mkoa wa Singida,Minde.
Baadhi ya wafanyakazi wa TANROADS mkoa wa Singida,waliohudhuria kilele cha maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani (mei mosi) yaliyofanyika kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida.

MKUU wa Mkoa wa Singida,Dk.Vicent Kone amewahimiza walimu,wazazi na walezi kuongeza juhudi katika kuwashawishi wanafunzi wengi zaidi kusomea masomo ya sayansi ili kama si kupunguza basi kulimaliza kabisa tatizo la uhaba wa walimu wa sayansi.

Dk.Kone ametoa wito huo hivi karibuni wakati akizungumza kwenye kilele cha sherehe za siku kuu ya wafanyakazi (Mei Mosi) duniani zilizofanyika kimkoa katika manispaa ya Singida.

Amesema kumekuwepo na kilio cha muda mrefu cha uhaba wa walimu wa masomo ya sanyansi katika shule karibu zote za sekondari mkoani na Tanzania kwa ujumla.


Amesema mwarubaini wa kulimaliza tatizo hilo ni kushawishi wanafunzi wengi kusoma masomo ya sayansi ili watakapohitimu warudi kuja kufundisha katika shule za hapa mkoani.

Aidha,Dk.Kone amewasisitiza wananchi waendelee  kuiunga mkono serikali katika kuimarisha na kuboresha sekta ya elimu nchini hususani katika kukamilisha ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara ya masomo ya kemia,fizikia na baolojia.

Katika hatua nyingine,Mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa madeni ya wafanyakazi wakiwemo walimu ya zaidi ya shilingi 2.2 bilioni,yanaendelea kuhakikiwa ili yaweze kulipwa.

Kwa upande wa wafanyakazi katika risala yao wamewaomba
wabunge wa bunge la katiba kupunguza malumbano na kejeli zisizo na tija na badala yake wazingatie jukumu lililowapeleka bungeni la kuwapatia wananchi katiba itakayokidhi mahitaji ya miaka 50 ijayo.

“Sisi wafanyakazi tunapendekeza katiba inayojali zaidi uhuru,usawa na haki swa ambazo binadamu anastahili kupata na kuepuka matabaka haswa ya vipato.Kuepuka ubepari kwa kujilimbikizia mali,ukabaila kwa kujichukulia ardhi kubwa na unyanyaji wa jasho la wafanyakazi na wakulima”,imesema sehemu ya risala hiyo.


Kauli mbiu ya mwaka huu ya mei mosi,ni ‘utawala bora utumike kutatua kero za wafanyakazi’.

No comments:

Post a Comment