Thursday, May 22, 2014

Kamanda wa UVCCM kata ya Kindai akabidhi vifaa vya michezo kwa vijana.

Kamanda wa (UVCCM) Kata ya Kindai, Omary Kinyeto (kushoto) akimkabidhi vifaa kwa Manahodha wa timu za soka ya Mperani Fc, Mahembe Fc, Munangi Boys na Kindai Boys  wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa kwa timu nne kwenye ofisi ya CCM ya Kata ya Kindai Manispaa Singida .
Kamanda wa (UVCCM) Kata ya Kindai, Omary Kinyeto akizungumza na vijana ofisi ya CCM Kata ya kindai Manispaa ya Singida.


VIJANA nchini wametakiwa kutambua kuwa hakuna biashara yenye kuingiza fedha nyingi popote duniani na kwa muda mfupi wa dakika tisini kama biashara ya kucheza mpira.

Changamoto hiyo imetolewa juzi mjini hapa na Kamanda wa Umoja wa Vijana (UVCCM)wa Kata ya Kindai Omary Salum ( Kinyeto) wakati akizungmza kwenye hafla fupi ya kukabishi vifaa vya michezo kwa timu nne za kata hiyo zitakazoshiriki ligi ya Kamanda Cup.

Kinyeto alisema kwa kutambua hivyo, vijana wamehimizwa kuzingatia michezo na kuithamini ili kupata ajira yenye kuingiza kipato kikubwa duniani kwa haraka zaidi.

“Ndugu zangu mimi haya mafanikio niliyonayo sasa ni kutokana na kucheza mpira, mimi nilikuwa mlinda mlango mahiri , kwa hiyo msinione nafanya haya mkadhani nafanya ilimradi tu, hii kitu mpira iko ndani ya damu yangu.” Alisema Kinyeto.

Aidha alisema anajitoa kwa hali na mali katika kuisaidia timu ya soka ya Singida United ambayo iko kwenye mashindano kituo cha Shinyanga, na kuwaomba wadau wengine kuisaidia timu hiyo.

Kinyeto alisema vifaa hivyo ambavyo ni
jezi seti nne, mipira minne, gloves  za walinda milango seti nne, zawadi mbalimbali na kombe vimemgharimu kiasi cha jumla ya shilingi milioni 2.5.

 Mshindi wa kwanza atapata shilingi laki moja pamoja na kombe ambapo mshindi wa pili atapata shilingi elfu hamsini.

Mapema Diwani wa Kata hiyo (CCM), Godfrey Solomon alimpongeza Kinyeto kwa kuona umihimu wa kuwakutanisha vijana hao kupitia michezo na kuwataka kuvitunza vifaa hivyo.

“Msije mkaanza kuingia viwanjani huku mkiwa mmekunywa viroba, mhesshimu haya mashindano, na baada ya kumalizika nisije kuona mtu amevaa jezi akiranda nayo mitaani, hizi jezi na vifaa mvitunze vitatusaidia baadae kwenye michezo mingine.” Alisema Solomon.

Jumla ya timu nne za Mahembe Fc, Kindai Boys, Munangi Fc, na Mperani Fc zinatarajiwa kushiriki michuano hiyo ya ligi inayotarajiwa kutimu vumbi leo kwenye viwanja vya shule ya sekondari Kindai.

No comments:

Post a Comment