Mkuu wa Wilaya ya Singida, Queen Mlozi.
MKUU wa Wilaya ya Singida,Queen Mlozi ameihimiza Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kujituma zaidi katika kuhakikisha mifuko mbalimbali ya hifadhi ya jamii inatoa taarifa sahihi kwa wananchi na wanachama watarajiwa juu ya haki zao kabla hawajajiunga.
Amedai kwamba wananchi na wanachama watarajiwa wakizitambua vema haki zao hizo watakuwa wamejengewa uwezo wa kufikia maamuzi sahihi katika kujiunga na mifuko hiyo ambayo Tanzania,ipo sita.
Mlozi ametoa rai hiyo hivi karibuni wakati akifungua semina ya siku moja iliyohusu uhabarisho wa shughuli za Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kwa wadau mbalimbali wa mkoa wa Singida.
Amesema kwa vile SSRA inasimamia mifuko yote hiyo sita ya hifadhi ya jamii ambayo ina mifuko tofauti tofauti ina jukumu kubwa la kusimamia mifuko hiyo inatoa taarifa za haki wanazopaswa kupewa wananchi na wanachama watarajiwa kabla ya kujiunga.
“Tumeshuhudia baadhi ya mifuko ikipewa fursa ya kuwaeleza wananchama watarajiwa shughuli zao na mafao wanayoyatoa,pindi watumishi hao wapya wakijiunga nayo”,amesema Mlozi na kuongeza;
“Hiyo ni hatua nzuri lakini usimamizi na ufuatiliaji zaidi unahitajika kutoka mamlaka ya usimamizi kwani mifuko hii ya hifadhi ya jamii inatofautiana kwa maana ya uzoefu,mtandao wa ofisi za matawi na watumishi na hata kwenye suala la uwekezaji”.
Akiijengea nguvu hoja yake hiyo, amesema suala la kutoa taarifa juu ya haki ya mwanachama mtarajiwa ni kwa mujibu wa sheria na 8 (nane) ya mwaka 2008 na kama ilivyorekebishwa mwaka 2012.
Amesema lengo kuu la sheria hiyo ni
kwamba waajiri wachache wenye tabia ya kuwarubuni na kupindisha sheria na kanuni wasipate mwanya wa kutimiza azma au malengo yao.
Kwa upande mjumbe wa Menejimenti na Mkuu wa Ununuzi SSRA, Emmanuel Urembo amesema kuwa hifadhi ya jamii ni haki ya kila mtu na haki hii imeainishwa katika ibara ya 11(1) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na sera ya taifa ya hifadhi ya jamii ya mwaka 2003.
“Haki hii pia imeainishwa kwenye mkataba wa kimataifa wa haki za binadamu wa mwaka 1948 pamoja na mikataba ya Shirika la Kazi Duniani (ILO). Hii ni pamoja na masuala yote ya msingi ya kijamii bila kujali hali ya kipato na michango yao au ajira”,amesema Urembo.
No comments:
Post a Comment