Thursday, May 22, 2014

Shanta yatoa leseni, Mtaji, huku Tan Discovery yakabidhi vifaa kwa kikundi cha uchimbaji wa Dhahabu cha Aminika Singida.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Manju Msambya akizungumza na wananchi wa kijiji cha Sambaru kwenye hafla hiyo ya makabidhiano ya leseni tatu.
Naibu Waziri wa Nishati na madini Steven Maselle akizungumza na wananchi wa kijiji cha Samabru Wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida wakati wa makabidhiano ya leseni tatu kwa wanakikundi cha Aminika Ltd.
Katibu wa kikundi cha Aminika Ltd akimkabidhi zawadi ya Mbuzi jike Naibu Waziri wa Nishati na madini Steven Maselle.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Steven Maselle akimkabidhi Mmoja ya wanakikundi Aminika Ltd cha kijiji cha Mang’onyi Wilayani Ikungi Sprian Danford ,moja ya leseni tatu za uchimbaji wa madini ya dhahabu zilizotolewa na Kampuni ya Shanta Mining Ltd, katika hafla fupi za makabidhiano iliyofanyika Kijiji cha Sambaru.


Kikundi cha ngoma ya Kinyaturu cha Muungano Ikungi wakitumbuiza kwenye sherehe za makabidhiano ya leseni.
Hapa mkuu wa kampuni ya kukopesha vifaa ya Tan Discovery Tanzania Roges Sezinga akitafsiri kwa lugha ya kishwahili kwa wananchi hotuba ya CEO wa Shanta.
 Huyu Afisa Mtendaji mkuu wa Kampuni ya Shanta Mining Ltd Tanzania, Mike Houston.
Katibu msaidizi wa chama cha wachimbaji wa madini mbalimbali mkoani singida John meta akiteta jambo na CEO wa Shanta  Mining Mike.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ikungi Hassan Tati akiagana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Maselle.

KAMPUNI ya uchimbaji wa madini ya dhahabu ya Shanta Mining Ltd, imetoa leseni tatu na mtaji wa shilingi milioni 40 kwa kikundi cha wachimbaji wadogo cha Aminika cha kijiji cha Mang’onyi  Wilayani Ikungi Mkoani Singida.

Kikundi hicho Aminika Gold Mine Co- Operative Society Ltd Mang’onyi kimekabidhiwa leseni hizo jana na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stepheni Maselle kwenye kijiji cha Sambaru.

Akikabidhi leseni hizo Naibu Waziri Maselle liwataka wanakikundi kujipanga vizuri katikakuanza kufanya kazi ya uchimbaji dhahabu ili kujikwamua kimaendeleo.


Aidha alisema ni matarajio yake kuona kuwa kikundi hicho kinakuwa na maendeleo na kuwa mfano wa kuigwa hapa nchini, kwani tayari nguvu kazi wamepewa mtaji na Shanta.

“Ndugu zangu sijui mungu awape nini, mmepewa leseni, mmepewa mtaji na vifaa vya kuanzia kazi na hawa wenzetu wa Tan Discovery, mnaoneshwa eneo ambalo tayari limefanyiwa utafiti, sasa kazi kwenu.” Alisema Maselle huku akishangiliwa na wananchi.

Aidha aliwataka wanakikundi hao kutumia kama SACCOS katika kukopa sehemu mbalimbali za kifedha kwa manufaa yetu na kizazi cha baadae.

Hata hivyo Naibu Waziri, Maselle alisema ni dhamira ya serikali kuendeleza wachimbaji wadogo hapa nchini, kwa kuwapatia mafunzo na namna bora ya uchimbaji madini.


Katika risala ya wanakikundi cha Aminika iliyosomwa na Katibu wake Hamis Kingi  alisema kikundi hicho ni  muungano wa vikundi  vitano kutoka vijiji   vitatu vitakavyoathirika na Mgodi wa Kampuni ya Shanta Mining vyenye jumla ya wanachama 218.

Kingi alivitaja vikundi hivyo kuwa ni Elimika  Sambaru,Amani Sambaru, Amka Sambaru, Aminifu Mang’onyi na Muungano Mlumbi ambavyo kwa pamoja vimeungana   na kuwa kikundi kimoja kinachojulikana kwa jina la Aminika

Aidha alitanabaisha kwamba vikundi  baada ya maelekezo  hayo   ya Serikali wachimbaji waliendelea kujiunga pamoja na kuunda  kikundi kilichofuata utaratibu wa kisheria wa kusajiliwa na kupata usajili namba, SIR624  Kikundi  cha Aminika Gold Mine  Co – Operative  Society Ltd – Mang’onyi  hatimaye  wamekabidhiwa   rasmi na Serikali.

“Mh,Naibu Waziri wa Nishati na Madini kwa kuwa kikundi  kiko Kisheria  tunaomba  Serikali  kupitia  Wizara yako ya Nishati na Madini Makubaliano yetu kati ya Kampuni na  Kikundi cha Aminika yaweze kutekelezeka  kwa muda  mwafaka, kwani  wanakikundi  wanahitaji kufanya  kazi  ili kujikwamua kiuchumi.”Alifafanua Kingi.


“Pia tunakushukuru wewe  binafsi kwa juhudi zako  kubwa kuwatetea  wachimbaji wadogo kwa kupitia Wizara ya Nishati na Madini.” Alisema.

No comments:

Post a Comment