Thursday, May 22, 2014

Waandishi wa habari wapewa changamoto ya ubunifu na kujituma.

Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa Singida,wakifuatilia mada   zilizokuwa zinatolewa na maafisa kutoka Mfuko wa Habari Tanzania (TMF) juu ya kuchangamkia ruzuku zinazotolewa na mfuko huo.
Afisa kutoka Mfuko wa Waandishi wa Habari Tanzania (TMF) Alex Kanyambo akitoa mada yake juu ya umuhimu wa vilabu vya waandishi wa habari kuchangamkia ruzuku zinazotolewa na TMF.Wa kwanza kushoto ni Afisa Habari wa TMF,Japhet Sanga na katikati ni Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida,Seif Takaza.
Afisa kutoka Mfuko wa Waandishi wa Habari Tanzania (TMF) Alex Kanyambo akitoa mada yake juu ya umuhimu wa vilabu vya waandishi wa habari kuchangamkia ruzuku zinazotolewa na TMF.Wa kwanza kushoto ni Afisa Habari wa TMF,Japhet Sanga na katikati ni Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari (Singpress) mkoa wa Singida,Seif Takaza.

WAANDISHI wa Habari mkoani Singida, wamehimizwa kuondokana na uandishi habari wa mazoea na badala yake wabadilike na kuwa wabunifu ili kazi yao iweze kukidhi viwango vya wakati uliopo.

Changamoto hiyo imetolewa hivi karibuni na mwandishi wa habari mkongwe, Eda Sanga wakati akizungmza kwenye semina ya Uhabarisho wa Mfuko wa Habari Tanzania (Tanzania Media Fund TMF) kwa waandishi wa habari mkoa wa Singida.

Amesema waandishi wa habari ule wa business as usual, haufai umepitwa na wakati unadumaza maendeleo ya mhusika.

amesema uandishi wa habari kwa sasa umetakiwa mwandishi wa habari ujitume, uwe mbunifu, ufanye uchunguzi wa kina ili ukiandika habari watu wakupongeze au wakusifu.

“Ninyi mnapaswa katika kutekeleza majukumu yenu muiangalie Singida kwa upana wake. Ni kero gani zinawasibu wananchi. Nini kifanyike ii kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu kero hizo”

Awali Afisa Habari wa TMF makao makuu,Japhet Sanga amewahimiza waandishi wa habari nchini kujenga utamaduni wa kuomba
uwezeshaji wa fedha kutoka TMF ili pamoja na mambo mengine kuongeza uzoefu zaidi katika kutekeleza majukumu yao.

Akifafanua, amesema TMF inatoa ruzuku ya fedha kwa ajili ya waandishi wa habari kuandika habari za uchunguzi ambazo zinaibua mambo mengi mapya na hasa kero zinazowakabili wananchi wakiwemo wa vijijini.

“TMF tunaamini kwamba kwa vyo vyote habari za uchuguzi zitamwezesha mwandishi husika kujifunza mambo mapya kwa hiyo atakuwa amepanua wigo wa ufahamu wa mambo mengi”.amesema.

No comments:

Post a Comment