Friday, April 11, 2014

Viongozi wanachangia kuporomoka kwa mchezo wa riadha nchini.

Mwanariadha mkongwe mkoani Singida, Pius Ikuu (68) akizungumza na mwakilishi wa mtandao wa Habari wa MOblog mkoa wa Singida, Nathaniel Limu. Mzee Ikuu katika enzi zake, amewahi kusinda medali mbili katika mchezo wa kukimbia mita 10,000 na tatu za mita 5,000.Pia maewahi kushiriki mashindano yaliyofanyika nchini Nageria (mwaka hakumbuki) na kushika nafasi ya saba.

KUPOROMOKA kwa mchezo wa riadha nchini kwa kiasi kikubwa imedaiwa kuwa kumechangiwa na viongozi walioko madarakani.

Akizungumza na MO blog hivi karibuni, mwanariadha aliyewahi kuwika kwenye mchezo huo katika miaka ya 60 mwishoni na mapema 1970,Pius Ikuu (78) amesema mchezo huo ambao una fursa kubwa kutoa nafasi kwa vijana wenye vipaji kujiajiri na kuajiriwa,kuachwa kutiliwa mkazo stahiki kuanzia ngazi ya shule za msingi na kusababisha upoteze mwelekeo.

Akifafanua zaidi,amesema uongozi hasa wa  ngazi ya taifa,umechangia kwa kiasi kikubwa kuuawa riadha  nchini,baada ya kuanza utamaduni wa kupendeleana katika maeneo ya mijini na kuyapa kisogo maeneo ya vijijini yaliyojaa vijana wenye vipaji vya riadha.

“Huyu Selemani Nyambui niliwahi kushiriki naye kwenye shindano la kukimbia mita 10,000 mwaka 1972 pale Dar-es-salaam.Katika uongozi wake kwa sasa hafanyi vizuri kwa sababu amesahau kuendeleza riadha kuanzia ngazi ya vijijini na shule za msingi,’ amesema.

Ikuu ambaye kwa sasa ni kiongozi wa kikundi cha uhamasishaji cha Chief Mpahi,amehimiza
ngazi mbalimbali za uongozi wa riadha nchini,kuweka mikakati madhubuti ya kufufua riadha kuanzia ngazi za chini,ili Tanzania iwezed kurejesha hadhi yake katika kufanya vizuri katika mashindano kuanzia ngazi ya kitaifa na kimataifa.

Mzee Ikuu katika enzi zake,amedai amewahi kushinda medali mbali za shaba za mbio za mita 10,000 na tatu za mita mia tano.


Pia ameshiriki mashindano ya riadha ya nchi za afrika yaliyofanyika nchini Nageria (mwaka amesahau) na akashika nafasi ya saba.

No comments:

Post a Comment