Sunday, April 14, 2013

Mtoto wa miaka minne alawitiwa na mwanafunzi wa sekondari, Mkoani Singida.

Kamanda mpya wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha), juu ya mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Chief Senge, kukamatwa kwa tuhuma ya kulawiti mtoto wa kiume wa miaka minne.

Jeshi  la polisi mkoa wa Singida linamshikilia mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Chief Senge mjini Singida Ibrahimu Saidi (17), kwa tuhuma ya kumwingilia kimwilia kinyume na maumbile  (kumlawiti) mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka minne (jina tunalo).
 Kamanda mpya wa jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP Geofrey Kamwela, amesema tukio hilo la kusikitisha limetokea Aprili 11 mwaka huu saa 11.30 jioni katika mtaa wa Majengo manispaa ya Singida.
Amesema mtuhumiwa ambaye ni mkazi wa kijiji cha Mtamaa manispaa ya Singida, amepanga nyumba moja na wazazi wa mwaathirika/mlalamikaji.
Kamanda Kamwela amesema mtoto aliyefanyiwa kitendo hicho cha kinyama alikuwa na mazoea ya kuingia chumbani kwa manafunzi huyo na hakukuwa na matatizo.
Amesema siku ya tukio, kama kawaida alipomwona mwanafunzi anaingia chumbani kwake, mtoto huyo naye alimfuata na kuingia chumbani humo.
Kamwela amesema mtoto huyo baada ya kuingia chumbani kwa mwanafunzi, mwanafunzi huyo alitumia

Saturday, April 13, 2013

Wakazi wa Utemini Singida wailalamikia manispaa kwa kutekelekeza barabara na kuzifanya kugeuka makorongo ya maji.



Barabara ya kuanzia klabu cha pombe za kienyeji cha Bulongwa kilichopo eneo la Utemini Singida mjini ikiwa imegeuka mto na kusababisha magari kushindwa kupita.

Wakazi  wa mtaa wa Utemini stesheni  Singida mjini wameilalamikia halmashauri ya manispaa ya Singida, kwa kitendo chake cha kuzitelekeza barabara za eneo hilo na kusababisha zigeuke kuwa mito yenye makorogo makubwa.
Wamedai kuwa mito na makorogo hayo yanatishia usalama wao kwa kiwango kuikubwa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wamedai kuwa barabara ya kuanzia

Friday, April 12, 2013

Serikali mkoa wa Singida yatenga maeneo rasmi kwa ajili ya wawekezaji.

 Mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi, (anayeangalia kamera) akizungumza kwenye mkutano kati yake, kaimu katibu mkuu wizara ya viwanda na biashara Dk.Shabani Mwinjaka na mwekezaji wa kiwanda cha ngozi Bw. Takuya  Miyaguchi.
 Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Dk.Shaban Mwinjaka (wa kwanza kushoto) Mwekezaji wa kiwanda cha ngozi mkoa wa Singida Bw. Takuya Miyaguchi na  Afisa Mipango wa halmashauri ya manispaa ya Singida, Godard Mwakalukwa wakifurahia jambo na mkuu wa wilaya ya Singida, mwalimu Queen Mlozi (hayupo kwenye picha).
 Kaimu katibu mkuu wizara ya viwanda na biashara, Dk.Shaban Mwinjak (wa pili kulia) akimwonyesha mwekezaji wa kiwanda cha ngozi Bw. Takuya Miyaguchi (wa kwanza kulia) eneo atakalojenga kiwanda chake cha ngozi katika kijiji Kisaki kitongoji cha Ng’aida manispaa ya Singida. Wa kwanza kushoto ni mshauri wa wizara ya viwanda na biashara na anayefuata ni Afisa Mipango wa manispaa ya Singida, Godard Mwakalukwa.
Mwekezaji wa kiwanda cha ngozi katika manispaa ya Singida Bw.Takuya Miyaguchi (aliyenyoosha mkono juu) akiangalia eneo atakalojenga kiwanda chake katika kijiji cha Kisaki kitongoji cha Ng’aida manispaa ya Singida. Kulia ni mshauri wa wizara ya viwanda na biashara kutoka serikali ya Japan.

Serikali  ya wilaya ya Singida imeiomba wizara ya viwanda na biashara iongeze kasi ya kuhamasisha wawekezaji wengi kuja mkoa wa Singida kwa madai kwamba mkoa una maeneo mengi ya kuwekeza.
Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi, wakati akizungumza kwenye mkutano wa pamoja kati yake, mwekezaji wa kiwanda cha ngozi na Kaimu Katibu Mkuu wa wizara ya viwanda na biashara Dk. Shaban Mwinjaka.
Amesema kwa upande wa wilaya yake wametenga eneo la

KIBONZO CHA LEO


Thursday, April 11, 2013

Mkuu wa wilaya ya Singida afanya ziara ya kukagua usafi kwenye soko la Vitunguu Misuna.

 Mkuu wa wilaya ya Singida, mwalimu Queen Mlozi (wa pili kulia) akizungumza na katibu wa soko la vitunguu Misuna, Jonathan Gunda Mtumba (kushoto aliyeshika vitunguu). Kitunguu chekundu  alichoshika DC Mlozi, ndivyo vyenye bei kubwa kuliko alivyoshika katibu Jonathan vyenye rangi ya kijivu.
 Baadhi ya wanawake wa manispaa ya Singida wamepata ajira ya muda ya kuchambua vitunguu na kuvijaza kwenye magunia kama wanavyoonekana kwenye picha.
Baadhi ya wafanyabishara makuli na vibarua wengine wa soko la vitunguu la Misuna walivyokutwa na mpiga picha wetu.
Mkuu wa wilaya ya Singida,mwalimu Queen Mlozi, akiwahimiza mama lishe wa soko la vitunguu la Misuna kudumisha usafi wakati wote ili kuondoa uwezekano wa kulipuka kwa magonjwa ya mlipuko ukiwemo kipindupindu.

CHEKI JINSI LORI LA MAFUTA LILIVYONUSURIKA KUZAMA MTO WAMI





Wednesday, April 10, 2013

Watu watatu wa familia moja wafariki,Mkoa Singida.

              Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP Linus Sinzumwa

Afisa upelelezi wa makosa ya jinai (RCO) mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka (wa kwanza kulia) 

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa polisi mkoa wa Singida ACP Linus Sinzumwa amesema kuwa Juma Rashidi Mkua (60), Johari Lazaro (45) na Amina Rashid mwenye umri wa mwaka moja na nusu, wote wa familia moja wamefariki dunia baada ya

Mtoto wa mwezi mmoja kuuawa na mama yake mzazi kwa kukatwa na panga kichwani,Singida.


 

VIKUNDI VYA KWAYA SINGIDA VYATAKIWA KULENGA KUIELIMISHA JAMII KUISHI MAISHA YA UADILIFU.


Kwaya ya Rivaivo inayomilkiwa na kanisa la Free Pentekoste Church la mjini Singida ikitoa burudani na kuelimisha wakati wa ibada ya Jumapili kanisa hapo.

Askofu wa kanisa la Free Pentekoste Church (FPCT) mkoani Singida Paulo Samwel amevitaka vikundi vya kwaya za injili, kujiwekea malengo ya kutoa huduma ya nyimbo za injili ndani na nje ya nchi.
Askofu Samweli ametoa changamoto hiyo wakati akitoa nasaha zake kwenye hafla iliyofana ya mazoezi ya kwaya ya Revaivoya mjini Singida, ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa kurekodi kanda yake ya DVD.
Amesema uzoefu unaonyesha wazi kuwa vikundi vya kwaya, vinafanya kazi nzuri ambazo ni pamoja na kuwahimiza na kuwahamasisha waumini kumcha Mungu na wakati huo huo, kuielimisha jamii kuishi maisha ya uadlifu kama njia mojawapo ya kudumisha amani na utulivu.
Ameisema vikundi vya kwaya pamoja na kutoa huduma nzuri kwa waumini, lakini pia

Tuesday, April 9, 2013

Polisi mkoani Singida yafanikiwa kumkamata mkulima akilimiki Bunduki ya Kijeshi aina ya SMG.

 Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida, ACP Linus Sinzumwa akitoa taarifa ya tukio la kukamata bunduki ya kijeshi SMG kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha). Bunduki hiyo inayodhaniwa kutumika kwenye matukio ya uhalifu, imekamatwa katika kijiji cha Mwamangembe jimbo la Manyoni magharibi.
Afisa upelelezi wa makosa ya jinai (RCO) mkoa wa Singida, Thobias Sedoyeka (wa kwanza kulia) akifuatilia taarifa ya kukamatwa kwa bunduki ya kijeshi aina ya SMG  iliyokuwa ikitolewa na kamanda wa polisi mkoa wa Singida,Linus Sinzumwa.

Jeshi la polisi mkoani Singida, limefanikiwa kukamata bunduki ya kijeshi aina ya SMG na risasi zake 28, inayodhaniwa kuwa hutumika katika matukio ya uhalifu.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida Linus Sinzumwa amesema bunduki hiyo wameikamata Aprili saba  saa saba usiku katika kijiji cha Mwamangembe tarafa ya Itigi jimbo la Manyoni magharibi.
Sinzumwa ambaye amehamishiwa mkoani Mtwara amesema kuwa wameikamata bunduki hiyo ambayo ilikuwa ikimilkiwa na mkulima John Bobo (46) mkazi wa kijiji cha Mitundu, jimbo la Manyoni magharibi.
Akifafanua amesema baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia mwema juu ya mtuhumiwa huyo kumiliki bunduki hiyo ya kijeshi, waliweka

Wilaya mpya ya Mkalama mkoani Singida yafanikiwa kuwapeleka shuleni wanafunzi 1,500 kati ya 1532.

Mkuu wa wilaya mpya ya Mkalama mkoani Singida, Edward Ole Lenga akihimiza shughuli za maendeleo katika mkutano wa hadhara uliofanyika  katika kijiji cha Gumanga kata ya Nduguti.

Wilaya mpya ya Mkalama mkoani Singida imefanikiwa kuwapelekea shuleni wanafunzi 1,500 ambao walikuwa hawajaripoti kuanza kidato cha kwanza mwaka huu katika shule walizopangiwa.
Hayo  yamesemwa na mkuu wa wilaya hiyo Edward Ole Lenga, wakati akizungumzia juu ya zoezi la kuwasaka wanafunzi 1,532 ambao hawakuripoti kuanza kidato cha kwanza Januari mwaka huu kama walivyopangiwa.
Amesema juhudi za makusudi zilizofanywa na viongozi na watendaji mbalimbali wa wilaya hiyo, zimefanikisha zoezi hilo la muda mfupi kwa asilimia kubwa.
Lenga amesema kazi bado inaendelea ya kuwasaka wanafunzi 32 ambao

MVUA KUBWA YASABABISHA KIFO CHA KIKONGWE NA WATU ZAIDI YA 7 KUKOSA MAKAZI SINGIDA.

 Mkuu wa wilaya ya Singida, mwalimu Queen Mlozi akizungumza na mwandishi wa habari wa Singida Yetu Blog ofisini kwake juu ya madhara makubwa yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha wilayani humo.
 Nguzo ya umeme iliyoangushwa katika mtaa wa Utemini stesheni  baada ya kunyesha kwa mvua kubwa iliyoambatana na upepe mkali.
 Mabati ya banda la maonyesho lililopo Mandewa nje kidogo ya Singida mjini, yakiwa juu ya mti baada ya kutupwa na upepo mkali wakati mvua kubwa ilionyesha siku ya Ijumaa.

Banda pekee la maonyesho lililopo Mandewa nje kidogo ya Singida mjini likiwa limeezuliwa mabati kwa upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa zilizonyesha Ijumaa jioni mjini Singida.

Picha juu na chini ni Nyumba iliyokuwa ikimilikiwa na kikongwe Isima Kituku @Nyamwantandu (86) iliyopo maeneo ya uwanja wa ndege wa jimbo la Singida mjini, baada ya kubomolewa na upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa. Kikongwe huyo alifariki dunia kwa kupigwa na radi wakati akikimbilia kwa jirani yake kujihifadhi.

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha wilayani Singida, zimesababisha madhara makubwa ikiwemo kikongwe mmoja mwenye umri wa miaka 86 kupigwa na radi, na kufariki dunia na pia wakazi wa nyumba saba kukosa makazi.
Mkuu wa wilaya ya Singida, Mwalimu Queen Mlozi amesema kuwa mvua hiyo kubwa mbaya ya hatari na yenye maji mengi, ilinyesha Ijumaa jioni kuanzia saa 2.15 hadi saa 3.45 usiku.
Amesema mvua hiyo iliambatana na upepo mkali, na  matukio ya mara kwa mara  ya radi kali ambayo yaliogofya sana wakazi wengi wilayani humo.
Amesema jumla ya

Monday, April 8, 2013

PICHA MBALIMBALI ZA MAAFA YA MVUA SINGIDA.





                                        

KESI YA VIGOGO WA CHADEMA KUNGURUMA LEO SINGIDA

Mshitakiwa wa kwanza katika kesi ya kumtolea lugha ya matusi mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi Mwita Waitara Mwakibe akitoka nje ya mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida

Kesi  inayowakabili vigogo wawili wa CHADEMA kwa tuhuma ya kumtolea lugha ya matusi mbunge wa jimbo la Iramba magharibi Mh. Lameck Mwigullu, inatarajiwa kuunguruma leo asubuhi kwenye mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida.
Kesi hiyo imeshindwa kuendelea kusikilizwa mara mbili baada ya

SHIDA YA MAJI SINGIDA SASA BASI...!

Tatizo sugu la upatikanaji wa maji kwa wakazi wa mji wa Singida, linatarajiwa kuwa historia kuanzia mwishoni mwa mwezi huu baada ya kukamilika kwa ujenzi wa mradi mkubwa wa maji unaofadhiliwa na benki ya waarabu (BADEA) kwa kushirikiana na umoja wa nchi zenye mafuta (OPEC). Baadhi ya vibarua  wakichimba mtaro wa kulaza mabomba ya maji ikiwa ni sehemu ya kumalizia ujenzi wa mradi mkubwa wa maji.

Tuesday, April 2, 2013

HIVI NDIVYO BAADHI YA WATU WALIVYOILA PASAKA SINGIDA




 Baadhi ya wakazi wa Singida mjini, wakipata chakula cha mchana siku ya pasaka kwa mama lishe wa kituo kikuu cha zamani cha mabasi mjini Singida, katika eneo la wazi kitendo ambacho si salama kwa afya zao.

Monday, April 1, 2013

Wakristo singida waungana na wenzao dunia nzima kuadhimisha sikukuu ya Pasaka.

Mchungaji wa kanisa la Free Pentekoste Church Tanzania (FPCT) mkoa wa Tanga,Steven Robert Mlenga,akihubiri waumini wa kanisa la FPCT Singida mjini  (31/3/2013) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku kuu ya Pasaka.
Baadhi ya waumini wa kanisa la FPCT Singida mjini, wakifuatilia kwa makini mahubiri yaliyokuwa yakitolewa na mchungaji Steven Robert Mlenga kutoka mkoa wa Tanga (hayupo kwenye picha) Mahubiri hayo yalikuwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku kuu ya Pasaka.
                                                   Wanakwaya wakifuatilia mahubiri.