Barabara ya kuanzia klabu cha pombe za kienyeji cha Bulongwa kilichopo eneo la Utemini Singida mjini ikiwa imegeuka mto na kusababisha magari kushindwa kupita.
Wakazi
wa mtaa wa Utemini stesheni Singida mjini wameilalamikia halmashauri
ya manispaa ya Singida, kwa kitendo chake cha kuzitelekeza barabara za
eneo hilo na kusababisha zigeuke kuwa mito yenye makorogo makubwa.
Wamedai kuwa mito na makorogo hayo yanatishia usalama wao kwa kiwango kuikubwa.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti, wamedai kuwa barabara ya kuanzia
klabu ya pombe za
kienyeji ya Bulongwa hadi nyumbani kwa Dk.Kiunsi, imegeuka kuwa mto
wenye makorongo makubwa na yenye kina kirefu.
Moja
wa wakazi hao Juma Kidimanda amesema licha ya kwamba maji ya mvua ya
mto huo yanaweza kusomba mtu/watu, pia inawawia vigumu watu wanaouguliwa
na wale wenye wajawazito kusafirisha ndugu zao hao kuwapeleka
hospitali.
Kwa
upande wake diwani wa kata ya Utemini Baltazari Kimario amekiri
kuharibika kwa barabara hiyo, lakini akadai kuwa hivi sasa TAMISEMI
imeahidi kuitengeneza kwa fedha zake.
Akifafanua,
amesema maafisa wa TAMISEMI wameshaikagua barabara hiyo na kuahidi
kuigharamia matengenezo yake pamoja na kuchimba mirefeji kwa pande zote
mbili.
Ndugu tunaomba picha nzuri nzuri za mjini Singida ili ipate kujulikana na watu wa nje wanafatilia mtandao wako itakua vizuri hivyo unatangazia mji wako.
ReplyDelete