Mshitakiwa wa kwanza katika
kesi ya kumtolea lugha ya matusi mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi
Mwita Waitara Mwakibe akitoka nje ya mahakama ya hakimu mkazi mjini
Singida
Kesi
inayowakabili vigogo wawili wa CHADEMA kwa tuhuma ya kumtolea lugha ya
matusi mbunge wa jimbo la Iramba magharibi Mh. Lameck Mwigullu,
inatarajiwa kuunguruma leo asubuhi kwenye mahakama ya hakimu mkazi mjini
Singida.
Kesi hiyo imeshindwa kuendelea kusikilizwa mara mbili baada ya
mashahidi wa upande wa mashitaka kushindwa kufika mahakamani.
Baada
ya mashahidi hao wa upande wa mashitaka kushindwa kufika mahakamani na
hakimu anayeisikiliza kesi hiyo Flora Ndale, aliagiza kuwa juhudi
zifanyike ili kuhakikisha kuwa mashahidi hao wanafika mahakamani hapo,
Aprili nane mwaka huu bila kukosa ili waweze kutoa ushahidi wao.
Hakimu
Ndale amesema kuwa kitendo cha mashahidi wa upande wa mashitaka
kutokufika mahakamani wakati washitakiwa kutoka Dar-es-salaam, wanafika
mahakamani hapo kila tarehe ya kesi ni usumbufu mkubwa kwa
washitakiwa,mawakili wao na wasikilizaji.
Vigogo
hao ambao wanatuhumiwa kumtolea lugha ya matusi mbunge wa jimbo la
Iramba magharibi Mh. Mwigulu Chemba ni Waitara Mwikwabe (37) Afisa Sera
na Utafiti makao makuu na Dk.Kitila Mkumbo Mhadhiri wa chuo kikuu
Dar-es-salaam na mshauri wa CHADEMA.
Vigogo hao wanatuhumiwa kutenda kosa hilo Julai 14 mwaka huu saa kumi jioni.
Kwa
mujiubu wa mwanasheria wa serikali Seif Ahmed, washitakiwa bila halali,
walimtusi mbunge Mwigullu kuwa ni malaya, mzinzi na mpumbavu huku
wakijuwa wazi kuwa kitendo hicho ni kinyume na sheria.
Seif
amesema kuwa washitakiwa hao bila halali, alitenda kosa hilo kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nguvumali kwa lengo la
viongozi wa CHADEMA kuzungumza na wananchi.
No comments:
Post a Comment