Mkuu wa wilaya ya Singida,
mwalimu Queen Mlozi akizungumza na mwandishi wa habari wa Singida Yetu Blog ofisini kwake juu
ya madhara makubwa yaliyosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha wilayani
humo.
Nguzo ya umeme iliyoangushwa katika mtaa wa Utemini stesheni baada ya kunyesha kwa mvua kubwa iliyoambatana na upepe mkali.
Mabati ya banda la maonyesho lililopo Mandewa nje kidogo ya Singida mjini, yakiwa juu ya mti baada ya kutupwa na upepo mkali wakati mvua kubwa ilionyesha siku ya Ijumaa.
Picha juu na chini ni Nyumba iliyokuwa ikimilikiwa na kikongwe Isima Kituku @Nyamwantandu (86) iliyopo maeneo ya uwanja wa ndege wa jimbo la Singida mjini, baada ya kubomolewa na upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa. Kikongwe huyo alifariki dunia kwa kupigwa na radi wakati akikimbilia kwa jirani yake kujihifadhi.

Banda
pekee la maonyesho lililopo Mandewa nje kidogo ya Singida mjini likiwa
limeezuliwa mabati kwa upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa
zilizonyesha Ijumaa jioni mjini Singida.
Picha juu na chini ni Nyumba iliyokuwa ikimilikiwa na kikongwe Isima Kituku @Nyamwantandu (86) iliyopo maeneo ya uwanja wa ndege wa jimbo la Singida mjini, baada ya kubomolewa na upepo mkali ulioambatana na mvua kubwa. Kikongwe huyo alifariki dunia kwa kupigwa na radi wakati akikimbilia kwa jirani yake kujihifadhi.
Mvua
kubwa zinazoendelea kunyesha wilayani Singida, zimesababisha madhara
makubwa ikiwemo kikongwe mmoja mwenye umri wa miaka 86 kupigwa na radi,
na kufariki dunia na pia wakazi wa nyumba saba kukosa makazi.
Mkuu
wa wilaya ya Singida, Mwalimu Queen Mlozi amesema kuwa mvua hiyo kubwa
mbaya ya hatari na yenye maji mengi, ilinyesha Ijumaa jioni kuanzia saa
2.15 hadi saa 3.45 usiku.
Amesema
mvua hiyo iliambatana na upepo mkali, na matukio ya mara kwa mara ya
radi kali ambayo yaliogofya sana wakazi wengi wilayani humo.
Amesema
jumla ya
nyumba saba, kanisa moja na kibanda cha maonyesho cha mkoa
kilichopo Mandewa nje kidogo ya mji wa Singida, zimeezuliwa mabati na
zingine zimeangushwa.
Mlozi
amesema katika matukio hayo, bibi kikongwe Isima Kitiku Nyamwantandu
(86) mkazi wa maeneo ya uwanja wa ndege mjini Singida, amefariki dunia
baada ya kupigwa na radi wakati anakimbilia kwa jirani yake kwenda
kujihifadhi, baada ya kuta za nyumba yake kubomolewa na upepo
ulioambatana na mvua hiyo.
“Nimefika
kwenye msiba wa bibi huyo na kutoa ubani kidogo.Lakini nilipoikagua
nyumba yake iliyobomolewa,niligundua kuwa haikuwa bora na ilijaa nyufa
kitendo ambacho kwa vyo vyote,kimechangia kuta za nyumba hiyo
kubomoka”amesema Mlozi.
Mkuu
huyo wa wilaya alisema kwa ujumla nyumba zote zilizoathirika na mvua
hiyo,karibu zote zilikuwa na mapungufu mengi kitendo kilichosababisha
mapaa yaezuliwe na kuta kuangushwa kirahisi.
“Nitumie
fursa hii kuwataka wakazi wa wilaya yangu kujenga utamaduni wa kukagua
nyumba zao na hasa zile za Tembe.Wahakikishe kama zipo imara kukabiliana
na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hivi sasa. Hofu yangu kubwa ipo
kwenye nyumba za matembe, hizi nyumba kuna wakati unafika miti
iliyotumika kujengea, huoza na hivyo inakuwa rahisi kuangushwa”amesema
mkuu huyo wa wilaya.
No comments:
Post a Comment