Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa polisi mkoa wa Singida
ACP Linus Sinzumwa, amesema mtoto Halawa Msika mkazi wa kijiji cha
Lugongo kata na tarafa ya Ibaga, aliuawa na mama yake mzazi Njile
Makelemo (40) kwa kumkatakata kichwani kwa panga na kusababisha kifo
chake papo hapo.
Amesema
tukio hilo la kusikitisha limetokea Aprili mosi mwaka huu saa tatu
usiku huko katika kijiji cha Lugongo wilaya mpya ya Mkalama.
Sinzumwa
amesema pia mama huyo anayedaiwa kuwa na matatizo ya akili, aliwajeruhi
watoto wake wengine Jandika Msika (2) na Hoga Msika (17) wote kwa
kuwakatwa panga katika mikono yao yote miwili.
Kamanda huyo amesema hivi sasa watoto hao wawili wamelazwa katika hospitali ya misheni Iyambi na hali zao sio nzuri.
Amesema
upelelezi wa awali umebaini kwamba mtuhumiwa huyo ana matatizo ya akili
na tayari ameisha kamatwa na anatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati
wowote upelelezi utakapo kamilika.
No comments:
Post a Comment