Kwaya ya Rivaivo inayomilkiwa na kanisa la Free Pentekoste Church la mjini Singida ikitoa burudani na kuelimisha wakati wa ibada ya Jumapili kanisa hapo.
Askofu
wa kanisa la Free Pentekoste Church (FPCT) mkoani Singida Paulo Samwel
amevitaka vikundi vya kwaya za injili, kujiwekea malengo ya kutoa huduma
ya nyimbo za injili ndani na nje ya nchi.
Askofu
Samweli ametoa changamoto hiyo wakati akitoa nasaha zake kwenye hafla
iliyofana ya mazoezi ya kwaya ya Revaivoya mjini Singida, ikiwa ni
sehemu ya mwendelezo wa kurekodi kanda yake ya DVD.
Amesema
uzoefu unaonyesha wazi kuwa vikundi vya kwaya, vinafanya kazi nzuri
ambazo ni pamoja na kuwahimiza na kuwahamasisha waumini kumcha Mungu na
wakati huo huo, kuielimisha jamii kuishi maisha ya uadlifu kama njia
mojawapo ya kudumisha amani na utulivu.
Ameisema vikundi vya kwaya pamoja na kutoa huduma nzuri kwa waumini,
lakini pia
vina wajibu wa kuihudumia jamii nyingine katika kuielimisha
juu ya umuhimu wa kuishi maisha ya uadilifu na kufanya kazi halali kwa
bidii ili kuboresha hali zao kiuchumi.
Kwa
hali hiyo, Askofu Samwel amesema kutokana na umuhimu huo, vikundi
vinapaswa kutoa huduma yao ndani na nje ya nchi, ili iweze kuwafikia
watu wengi zaidi wenye tamaduni tofauti tofauti.
No comments:
Post a Comment