Saturday, December 8, 2012

Madhehebu ya dini jimbo la Singida yamtwisha mgana msindai mzigo wa kutokomeza rushwa ndani ya CCM.

 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mgana Izumbe Msindai akizungumza kwenye mkutano wa viongozi wa madhehebu ya dini jimbo la Singida mjini.Kushoto ni mwenyekiti wa CCM jimbo la Singida mjini Hamisi Nguli na wa pili kulia ni katibu wa CCM mkoa wa Singida,Naomi Kapambala.
 Mmoja wa viongozi wa madhahebu ya dini,mzee Omari Hamza akitoa kero alizokuwa nazo kwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindai (hayupo kwenye picha).
Baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini waliohudhuria mkutano ulioitishwa kwa ajili ya mwenyekiti wa CCM mkoa kujitambulisha kwao na wao kutoa kero ushauri ya maoni kwa lengo la kuendeleza manispaa ya Singida.


Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini jimbo la Singida mjini wamemwomba Mwenyekiti mpya wa CCM  mkoa wa Singida Mgana Izumbe Msindai, kuweka mikakati madhubuti itakayokomesha vitendo vyote vya rushwa ili
pamoja na mambo mengine, kurejesha imani ya wanaCCM na wananchi kwa ujumla kwa chama chao kikongwe.
Viongozi hao wamemtwisha Msindai mzigo huo wa kukomesha vitendo vya rushwa ndani ya CCM, wakati wakizungumza kwenye mkutano ulioitishwa kwa ajili ya viongozi wa madhehebu ya dini kufahamiana na Mwenyekiti Msindai na pia kutoa kero, ushauri na maoni yao kwa lengo la kuboresha maendeleo ya jimbo la Singida mjini na mkoa kwa ujumla.
Wamedai kuwa nguvu kubwa ya CCM iliyokuwepo katika miaka mingi ya nyuma ambayo imeendelea kudumisha amani na utulivu, hivi sasa imeanza kuwa shakani kutokana na kukithiri kwa vitendo vya rushwa na mambo mengine.
Aidha, viongozi hao wameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kufundisha na kuajiri walimu maalum ambaokazi yao itakuwa kufundisha masuala ya dini ili kupunguza kasi kubwa ya mmomonyoko wa maadili iliyopo hivi sasa.
Kwa upande wake Mwenyekiti Msindai,amesema mkutano huo ni mwendelezo wa hatua yake ya kukutana na makundi mbalimbali kwa lengo la kupata ushauri, maoni na kero zinazowakabili wananchi.

No comments:

Post a Comment