Mkuu wa mkoa wa Singida
Dk.Parseko Kone akizungumza kwenye mkutano maalum wa uhabarishaji juu ya
umuhimu wa chanjo mpya za Rotavirus inayokinga maradhi ya kuharisha na
PCV 13,inayokinga ugonjwa wa Nimonia.Chanjo hizo ambazo ni
mpya,zinatarajiwa kuanza kutolewa kuanzia Januari mwakani.
Mkuu wa wilaya ya Iramba.Yahaya Nawanda akichingia mada juu ya chanjo mpya za totavirus na PCV 13 kwenye mkutano maalum kwa lengo la kuhabarisha juu ya chanjo hizo.
Mkuu wa wilaya ya Iramba.Yahaya Nawanda akichingia mada juu ya chanjo mpya za totavirus na PCV 13 kwenye mkutano maalum kwa lengo la kuhabarisha juu ya chanjo hizo.
Mkuu
wa mkoa wa Singida Dkt. Parseko Kone amewaagiza wakuu wa wilaya
kuhakikisha wanawahamasisha wananchi juu ya umuhimu wa watoto wao kupata
chanjo mbili mpya, za Rotavirus na PCV 13 ili kujikinga na magonjwa ya
kuharisha na nimonia.
Dk.
Kone ametoa agiza hilo wakati akizungumza kwenye mkutano maalum
ulioitishwa kwa ajili ya uhabarishaji wa chanjo hizo mpya, ambapo
amesema lengo la serikali kupitia wizara yake ya afya na ustawi wa jamii
ni kuhakikisha wananchi wake wanakuwa na afya bora.
Mkuu
huyo wa mkoa amesema ili lengo hilo liweze kufanikiwa, imeanzisha
chanjo mpya ya Rotavirus ambayo ni kwa ajili ya kukinga magonjwa ya
kuharisha na PCV 13 ya kuzuia nimonia kwa watoto wote walio chini ya
umri wa chini ya mwaka moja.
Amesema chanjo hizo zinatarajiwa kuanza kutolewa kuanzia Januari mwakani, na zitatolwewa kwenye kliniki zote.
Akifafanua zaidi, amesema kuharisha kunakosababishwa na virus vya rota, kunazuilika kwa chanjo inayoitwa Rotavirus.
Kuhusu
chanjo ya PCV 13, amesema chanjo hiyo inayo uwezo wa kuzuia magonjwa
hatari yakiwemo homa ya kichomi (nimonia) na uti wa mgongo.
No comments:
Post a Comment