Afisa msimamizi wa kampuni ya Tan Discovery Akida Sungura akiwa Internet Cafe akitekeleza majukumu yake.
Kampuni
ya Tan Discovery inayojishughulisha na kuuza na kukodisha vifaa vya
uchimbaji madini kwa wachimbaji wadogo mkoani Singida, imekanusha
taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kwamba haijawasaidia
wachimbaji kufikia
malengo yao.
malengo yao.
Msimamizi
wa kituo cha Tan Discovery mkoani Singida Akida Sungura, amesema
taarifa hizo hazina ukweli wo wote kwani kampuni toka imefungua kituo
katika kijiji cha London wilaya ya Manyoni, imeuza kwa bei nafuu vifaa
vingi kwa lengo la kuwaendeleza wachimbaji wadogo.
Amesema
pia kituo hicho kimekodisha na kinaendelea kukodisha vifaa mbalimbali
kwa wachimbaji wadogo kwa gharama ndogo kadri ya mahitaji yao.
Amesema
Kampuni hiyo pamoja na kuuza na kukodisha vifaa kwa wachimbaji wadogo,
pia imeweza kuleta wataalam wa madini kutoka Dodoma na wakatoa mafunzo
ya kina kwa wachimbaji, lengo likiwa ni kupanua uwezo wao kuhusu
uchimbaji na kubaini miamba yenye dhahabu.
Aidha,
msimamizi huyo amesema gharama za kuuza na kukodisha vifaa
walivyonavyo, sio kubwa kama inavyodaiwa na wachimbaji wadogo wa mkoa wa
Singida.
“Mimi
nitoe wito tu kwa ndugu zangu wachimbaji wadogo, kwamba kazi ya
uchimbaji madini, ni kazi nzito na ni ya gharama kubwa.Si rahisi kwa
mchimbaji mmoja mmoja kuimudu”alifafanua Sungura.
Amesema
dawa pekee ya wachimbaji wadogo kumudu kazi ya uchimbaji ni kujiunga
kwenye vikundi ili kuwa na nguvu ya kutosha na wakati huo huo,
kujijengea mazingira mazuri ya kuweza kukopesheka na taasisi za kifedha.
Katika hatua nyingine, Sungura pia amekanusha taarifa kwamba kampuni yao imekopeshwa na serikali zaidi ya shilingi bilioni nane.
Msimamizi
huyo amesisitiza kuwa Serikali haijatupa shilingi bilioni nane, imetupa
shilingi milioni 180 tu hadi sasa. Baadaye inatarajia kutuongeza
shilingi milioni 20. Kwa ujumla shilingi milioni 200 ni fedha chache mno
kwenye shughuli ya madin.
Sungura
amesema serikali itakapoongeza kiwango kizuri zaidi cha fedha kwa maana
ya kutosheleza mahitaji, kampuni ya Tan Discovery, nayo itajitahidi
kukidhi mahitaji ya wachimbaji wote wadogo wa mkoa wa Singida.
Katika
risala ya hivi karibuni ya chama cha watafiti na wachimbaji madini mkoa
wa Singida (SIREMA), imedai kwamba kampuni ya Tan Discovery, gharama
zake za kukodisha na kuuza vifaa ni kubwa mno na wachimbaji wadogo
hawawezi kuimudu.
No comments:
Post a Comment