Vigogo wa CHADEMA Dkt. Kitila
Mkumbo mshauri wa CHADEMA na mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar-es-salaam
(kulia) katibu wa sera na utafiti wa CHADEMA makao makuu Mwita Waitara
(katikati) na Pela Ngunangwa aliyejitambulisha kuwa ni dereva kiongozi
ofisi za CHADEMA makao makuu, wakiwa wanaelekea kuingia kwenye mahakama
ya hakimu mkazi mjini Singida.
Wakili wa vigogo wa CHADEMA Raymond Kimu (wa kwanza kushoto aliyenyoosha kidole) akiteta na wateja wake Mwita Waitara (katikati) na wa pili kulia mwenye miwani Dk.Kitila Mkumbo.
Kesi inayowakabili vigogo wa CHADEMA ya kumtolea lugha ya matusi mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi (CCM) Mwigulu Lameck Nchemba, iliyoanza kusikilizwa jana kwenye mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida imeahirishwa hadi leo.
Wakili wa vigogo wa CHADEMA Raymond Kimu (wa kwanza kushoto aliyenyoosha kidole) akiteta na wateja wake Mwita Waitara (katikati) na wa pili kulia mwenye miwani Dk.Kitila Mkumbo.
Kesi inayowakabili vigogo wa CHADEMA ya kumtolea lugha ya matusi mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi (CCM) Mwigulu Lameck Nchemba, iliyoanza kusikilizwa jana kwenye mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida imeahirishwa hadi leo.
Kesi hiyo imeahirishwa baada ya kukosekana kwa hati za
maelezo ya awali yalioandikwa polisi na mashahidi wa upande wa mashitaka.
Vigogo
wanaokabiliwa na kesi hiyo ni katibu wa Sera na Utafiti wa CHADEMA
Makao Makuu Mwita Waitara na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam
na Mshauri wa CHADEMA Dkt. Kitila Mkumbo.
Baada
ya shahidi wa pili Lyanga Elikana kuanza kutoa ushahidi wake huku
akiongozwa na mwendesha mashitaka mkaguzi msaidizi wa polisi Shukrani
Magafu, wakili wa upande wa washitakiwa Tundu Lissu, alisimama na kuomba
maelezo ya shahidi aliyoyaandika polisi awali.
Mwendesha
mashitaka Magafu, alisema kuwa kwa wakati huo hana hayo maelezo na
kuiomba mahakama iliyokuwa chini ya hakimu Ruth Massamu, kuahirisha
kesi hiyo hadi leo atakapoleta maelezo ya shahidi Lyanga pamoja na
mashahidi wengine wanne waliobakia.
Mahakama ilikubaliana na ombi hilo ambalo pia upande wa utetezi ulikubaliana.
Awali
shahidi Lyanga alihojiwa na Tundu Lissu kama ilifuatavyo; shahidi,je ni
kweli mshitakiwa wa kwanza Waitara, aliuliza wananchi waliokuwa
wamehudhuria mkutano wa hadhara kama wanamfahamu ‘the comedy’ wa jimbo
la Iramba magharibi?
Shahidi Lyanga alijibu “ni kweli Waitara aliuliza swali hilo ambalo lilijibiwa na wananchi kuwa ‘ndio’ wanamfahamu.
Tundu, hebu mweleze mheshimiwa hakimu na wasikilizaji wa kesi hii, wananchi walijibu kuwa ni nani huyo ‘the comedy’.
Shahidi Lyanga alijibu kuwa wananchi walimjibu Waitara kuwa ‘the comedy’huyo ni Mwigullu Nchemba.
Tundu
aliuliza tena kuwa watu wanaofanya vichekesho yaani the comedy kama
akina Masaja, je sanaa hiyo inakashifu au inatukana watu.
Shahidi Lyanga, sio kashifa ila ikitumiwa vibaya, inakuwa kashifa na matusi.
Aidha
shahidi Lyanga aliiambia mahakama hiyo kuwa matusi yaliyotolewa na
mshitakiwa Waitara kuwa mbunge wa jimbo la Iramba magharibi Mwigulu, ni
mzizi, Malaya, mpumbavu na fisadi, yalirudiwa kutamkwa na mshitakiwa wa
pili ambaye ni Dk.Kitila Mkumbo.
Washitakiwa
hao wadaiwa kutenda kosa hilo Julai 14 mwaka huu katika kijiji cha
Nguvumali kata ya Ndago jimbo la Iramba magharibi.
Washitakiwa
hao wanatetewa na wakili Tundu Lissu, Onesmo Kyaule (mkazi wa jijini
Dar-es-salaam ) na Raymond Kimu wa Singida mjini.
No comments:
Post a Comment