Maafisa TFDA kanda ya kati,
Florent Kyombo (kushoto) akishuhudia mmiliki wa duka la Temba, Singida
mjini Bw. Temba akisaini fomu yakutekeza bidhaa zilizoisha muda wake na
akazitoa dukani, TFDA walimsifu sana.
Kaimu meneja TFDA kanda kati, Florent Kyombo na Joseph Mwasambili wakikagua vinywaji vikali kwenye moja ya duka mjini Singida, katika oparesheni maalumu kusaka bidhaa zilizomaliza muda kwa matumizi ya binadamu.
Kaimu meneja TFDA kanda kati, Florent Kyombo na Joseph Mwasambili wakikagua vinywaji vikali kwenye moja ya duka mjini Singida, katika oparesheni maalumu kusaka bidhaa zilizomaliza muda kwa matumizi ya binadamu.
Mamlaka
ya chakula na dawa nchini (TFDA), imekamata bidhaa mbalimbali ikiwemo
vipodozi vilivyopigwa marufuku na vilivyomaliza muda vikiwa na thamani
ya zaidi ya Sh. Milioni
2.6, mjini Singida.
Kukamatwa
kwa bidhaa hizo, kumefuatia zoezi maalumu la oparesheni iliyofanyika
katika maduka mbalimbali yanayouza bidhaa hizo, katika manispaa ya
Singida.
Akizungumza
na Singida Yetu Blog kaimu meneja wa TFDA kanda ya kati, Florent Kyombo amesema
bidhaa hizo zilikamatwa na maafisa wa mamlaka hiyo, kanda ya kati, kwa
kushirikiana na wenzao wa manispaa Singida.
Kyombo
amesema, katika operesheni hiyo jumla ya kilo 112.2 za vipodozi na
vyakula visivyoruhusiwa kwa matumizi ya binadamu vilikamatwa.
Hata
hivyo Kyombo akieleza kuridhishwa na mwamko wa wananchi na wamiliki wa
biashara hizo katika mji wa Singida, kwa madai kuwa hivi sasa
wanajitahidi kufuata sheria, kanuni na taratibu za TFDA.
“Wamiliki
wa maduka hivi sasa wanajitahidi kufuata sheria za TFDA, bidhaa
ikimaliza muda utakuta imeondolewa sehemu ya kuuzia, hadi chumba
maalumu, tayari kwa ajili ya maafisa wa TFDA kukagua na
kuteketezwa,”amesema.
Aliongeza
operesheni hiyo iliyoanza desemba 10, 2012 mjini Singida, imeendelea
hadi jana Desemba 15 mwaka huu, kabla ya kuendelea Singida vijijini na
baadaye kumalizia katika wilayani Iramba.
Kyombo
amesema hadi kufikia juzi jumatano ya tarehe 12, tayari maduka 64
yanayojihusisha na uuzaji vipodozi, dawa na vyakula yalikwishafanyiwa
ukaguzi.
“Nashukuru
wamiliki wa maduka ya vipodi, dawa na chakula wanatuelewa… sheria
inafuatwa sana na ukiukwaji umepungua kwa asilimia kubwa sana
ikilinganishwa na hapo mwanzo,”alifafanua.
Aidha
Kyombo ametumia fursa hiyo kuwataka wamiliki na watumiaji kuchukua
tahadhari kwa kusoma muda wa bidhaa kutengenezwa na muda wa kuharibika,
kila wanaponunua bidhaa katika maduka mbalimbali.
“Jamii
iwe makini na bidhaa wanazonunua…vipodozi vilivyopigwa marufuku vina
madhara makubwa sana, vinasababisha kansa ya figo na ngozi, kwa kweli
zinaharibu ngozi, naomba wananchi wawe makini sana,”amesema Kyombo.
No comments:
Post a Comment