Mkufunzi Mnaku Ambani akitoa
mafunzo ya biashara na uchumi yaliyohudhuriwa na waandishi wa habari 17
wa mkoa wa Singida. Mafunzo hayo ya siku nne yalifanyika kwenye ukumbi
wa mikutano wa kanisa katoliki mjini Singida.
Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa Singida wakimsikiliza kwa makini mkufunzi Mnaku Ambani (hayupo kwenye picha) akitoa mada zake za biashara na uchumi.
Wanachama wa klabu ya waandishi wa habari mkoani Singida(Singpress), wamehimizwa kufanya juhudi za makusudi kumiliki ardhi ili pamoja na mambo mengine, kujijengea mazingira mazuri ya
kuboresha uchumi wao.

Wito
huo umetolewa na mwezeshaji wa mafunzo ya biashara na uchumi Mnaku
Ambani, yaliyohudhuriwa na waandishi wa habari 17 wa mkoa huu.
Amesema
ardhi kwa sasa ni rasilimali ambayo mahitaji yake yanazidi kuongezeka
kwa kasi kubwa, kutokana na hali hiyo, hata thamani yake nayo inazidi
kuongezeka pia kwa kasi.
Katika
hatua nyingine Ambani amewataka waandishi wa habari kuongeza kasi
katika kujielimisha kwa bidii, iwe kwa kwenda shule au kujisomea
nyumbani.
Amesema
mambo mengi sasa duniani yanabadilika kila kukicha yakiwemo ya
teknolojia, kwa hiyo, ili kukabiliana na mabadiliko hayo,ni lazima
mwandishi wa habari ujitume katika kujiendeleza kielimu.
Ambani
amewataka wasiridhike na elimu waliyonayo na watambue kwamba bado
wanayo safari ndefu ya kujielimisha ili waweze kwenda na wakati.
Mafunzo
hayo ya siku nne yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa
katoliki mjini Singida, yaliandaliwa na Singpress na kufadhiliwa na
Umoja wa vilabu vya waandishi wa habari (UTPCT) nchini wenye makazi yake
jijini Mwanza.
No comments:
Post a Comment